Mkurugenzi Mtendaji wa Gihon Ministry, Rebecca Stanford (kushoto), akiwa na Mwanasheria wa Gihon, Monica Mhoja wakati walipokwenda ofisi ya Balozi wa Malawi nchini.
Mwakilishi wa Balozi wa Malawi nchini, Micharl Gama (kulia), akiwa na viongozi wa Huduma ya Kiroho ya Gihon ofisi ya ubalozi huo hapa nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gihon Ministry, Rebecca Stanford, Mwanasheria wa Gihon, Monica Mhoja, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Gihon, Leonce Zimbandu na Ofisa Habari, Michael Malanyingi.
Mwakilishi wa Balozi wa Malawi nchini, Micharl Gama (kulia), akiwa na viongozi wa Huduma ya Kiroho ya Gihon ofisi ya ubalozi huo hapa nchini. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Gihon Ministry, Rebecca Stanford, Mwanasheria wa Gihon, Monica Mhoja, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Gihon, Leonce Zimbandu
Mwandishi wetu
OFISI ya Ubalozi wa
Malawi nchini imeushauri uongozi wa huduma ya Gihon kuwasiliana na Bodi ya
usajili ya Malawi kabla ya kujaza fomu ya maombi ya usajili wa huduma hiyo.
Lengo ni kuutaka
uongozi huo kufahamu sheria za usajili za nchini Malawi ili kuepuka usumbufu
ambao unaweza kujitokeza iwapo fomu zitajazwa bila kuzingatia sheria na
taratibu za nchi husika.
Katibu wa Balozi
wa Malawi nchini,Micharl Gama aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na uongozi
wa Gihon, jana katika ofisi ya ubalozi huo ili kupata ufafanuzi wa namna
ya kufungua huduma hiyo nchini Malawi.
Alisema ubalozi
utahakikisha mawasiliano yanapatikana ili mwanasheria kutoka bodi ya usajili ya
Malawi kutoa maelekezo yanayotakiwa kufuatwa kabla ya kufanya usajili wa
taasisi (NGO).
“Unajua mimi
siyo mtaalamu wa masuala ya sheria, hivyo mawasiliano nitakayowapatia
yatafafanua vizuri kifungu cha sheria namba 5.05 cha Malawi,” alisema.
Alisema wajibu wa
ofisi hiyo ya ubalozi ni kuwaunganisha na wenye mamlaka ili waweze kutekeleza
wajibu wao wa kisheria, hivyo hana uwezo wa tafsiri sharia ya usajili wa
NGO.
Mwanasheria wa
huduma ya Gihon,Monica Mhoja alisema kuwa huduma hiyo imeona kabla ya kujaza
fomu za usajili wa huduma hiyo ya kiroho nchini Malawi, waliamua
kuomba ushauri kutoka katika ofisi za ubalozi huo.
Alisema taratibu zipo
tofauti kati ya nchi moja na nyingine, hivyo itakuwa busara kufahamu sheria za
usajili kutoka nchini Malawi ili kuepuka uvunjaji wa taratibu za kisheria.
“Tunaomba kufahamu
taratibu za usajili wa NGO zilizopo nchini Malawi, kwani tunahitaji kufungua
huduma ili kufahamu mgawanyo wa madaraka ulivyo kabla ya huduma kuanza
kisheria,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa
huduma ya Gihon nchini, Rebecca Stanford alisema wamefikia uamuzi wa
kushughulikia usajili nchini Malawi baada ya watu hao kubarikiwa
huduma hiyo kiroho na kimwili.
“Tayari tumefungua
tawi la huduma ya Gihon nchini Malawi kwa muda wa miaka miwili,
hivyo kutokana na uhitaji uliopo tumeona tuisajili huduma hiyo ili itambulike
rasmi,” alisema.
No comments:
Post a Comment