Meneja Masoko la Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe (katikati), akizungumza katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano wa tisa wa LAPF utakaofanyika Machi 9 na 10, 2017 Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Kulia ni Meneja wa Takwimu Hadhari na Tathmini wa LAPF, Abubakar Ndwata na Ofisa Masoko na Mawasiliano wa LAPF, Rehema Mkamba.
Meneja wa Takwimu Hadhari na Tathmini wa LAPF, Abubakar Ndwata (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Meneja Masoko la Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.
Na Christina Mseja
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kufungua mkutano wa tisa wa wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF jijini Arusha.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Meneja Masoko la Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe alisema mkutano huo utafanyika kwa siku mbili Machi tisa na 10 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Alisema lengo la mkutano huo ni kutoa za uendeshaji wa Mfuko na kuwapa fursa wadau kutoa maoni yao mbalimbali ili kuboresha utendaji wa mfuko.
"Mikutano hii hufanyika ili kutekeleza maagizo ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA) " alisema Mlowe.
Alisema kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni "Kuibua Fursa Endelevu za Ajira kwa maendeleo ya Jamii Tanzania"
Aliongeza kuwa pamoja na mambo mengine kwenye mkutano huo mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo mada inayohusu kauli mbiu iliyotajwa.
Mada nyingine zitahusu utendaji wa mfuko kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na taarifa ya uwekeza pamoja na taarifa ya Hesabu za Mfuko kwa mwaka 2015/2016.
Alisema siku ya kwanza ya ufunguzi wa mkutano LAPF itazindua huduma ya mkopo wa kujikimu ijulikanayo kwa jina la Maisha popote na LAPF kwa kushirikiana na benki ya CRDB .
"Huduma hii imewanufaisha sana wanachama wa mfuko wanaonza ajira kwa kuwapa fursa ya kukopa mara tatu ya mshahara wao kukidhi mahitaji ya awali kama kulipa pango,nk kwa riba nafuu"
Aliongeza kuwa ufunguzi wa mkutano huo tarehe 9 machi,2017 itakuwa siku ya maadhimmishi ya figo duniani hivyo LAPF itatumia siku hiyo kuwapa fursa wadau wote watakao shiriki mkutano huu kupima figo kwa kushirikiana na watalaamu kutoka Hopstali ya KCMC.
LAPF inatarajia kupata washiriki zaidi ya 600 katika mkutano huu kwa kuzingatia idadi ya waalikwa.
Meneja wa Takwimu Hadhari na Tathmini wa LAPF, Abubakar Ndwata alisema kwa mwaka wa fedha wa 2015-2016 mafao yaliokusanywa ni sh. bilioni 107.25 na sh. bilion 2 kwa ajili ya mafao ya uzazi.
No comments:
Post a Comment