Waandaaji wa Tuzo za Kimataifa
za Mitaji kwa Wajasirimali wadogo na wa Kati kwa kushirikiana na Nchi za
G20, Shirika la IFC (mwanachama wa Benki ya Dunia) pamoja na Jukwaa la
Kufadhili Ujasiriamali (SME Finance Forum) mwaka huu wameanzisha
kipengele kipya cha Hati Fungani Endelevu ya Mwaka kuzitunuku Taasisi
zinazofanya vizuri kwenye eneo hilo.
Hati Fungani ya NMB JASIRI
ndiyo imechaguliwa kama mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo mpya. Ushindi huo
umepatikana baada ya Hati Fungani hiyo kupitiwa na jopo la majaji zaidi
ya 100 waliovutiwa na mlengo wake, muundo na uwezo wa kulihudumia
kifedha kundi ambalo halizingatiwi kwa Mitaji ya kawaida iliyozoeleka.
Chanzo
hiki cha Mtaji kinaendana vyema na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya
Umoja wa Mataifa na Kanuni za Dhamana za Kijamii za Chama cha Kimataifa
cha Masoko ya Mitaji.
Katika hotuba yake ya kukubali tuzo na
heshima hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi Ruth Zaipuna,
alisema: “Sisi NMB tumejitolea kuhakikisha tasnia ya fedha inachangia
maendeleo ya Tanzania. Hati Fungani ya JASIRI yenye lengo la kupunguza
pengo la Mitaji linalozikabili biashara ndogo ndogo na za kati
zinazomilikiwa au kusimamiwa na akinamama ni keielelezo kizuri cha
dhamira hii.”
Hati Fungani yetu imefanikiwa kupata matokeo
yaliyotarajiwa ya kusaidia kuwawezesha wanawake kiuchumi na
kushughulikia madhumuni matatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo
ni lengo la kwanza, la tano na la kumi.
“Tuzo hii ni wakati
muafaka wa kihistoria kwa sekta ya benki nchini, kwani inaiweka nchi
yetu katika ramani ya dunia kwa uongozi kwenye Mitaji endelevu. Hati
Fungani ya JASIRI inaweka kigezo kipya nchini na barani Afrika katika
kukuza vyanzo vingine vya Mitaji mbadala kwa ajili ya wawekezaji wa
ndani na wakimataifa,” aliongeza.
Bi Zaipuna amesema tuzo hiyo ni
kwa ajilia wa wafanyakazi wote wa NMB, washirika wake, wawekezaji na
wasimamizi wa sekta ya fedha kwa kuchangia mafanikio makubwa ya dhamana
ya JASIRI.Mhazini
wa Benki ya NMB – Aziz Chacha (Kushoto) akipokea tuzo ya Hati Fungani
Bora ya Mwaka 2022 kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Ufadhili
wa Ujasiriamali (SME Finance Forum) – Mathew Gamser kwenye hafla ya tuzo
iliyoandaliwa na Waandaaji wa Tuzo za Kimataifa za Mitaji kwa
Wajasirimali Wadogo na wa Kati kwa kushirikiana na Nchi za G20, Shirika
la IFC(mwanachama wa Benki ya Dunia) pamoja na Jukwaa la Kufadhili
Ujasiriamali (SME Finance Forum) jijini Phnom Penh, Cambodia. Benki ya
NMB kupitia hatifungani yake ya NMB Jasiri imeshinda tuzo ya ‘Platinum’
Upande wa Kundi la Dhamana Endelevu ya Mwaka Kwenye Tuzo za Ufadhili wa
Ujasiriamali za Mwaka 2022.
Thursday, September 22, 2022
New
NMB Jasiri Bond - Hati Fungani Bora ya Mwaka 2022 Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment