Na Mwandishi Wetu-KIGALI,RWANDA
MKURUGENZI
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA)
Mhandisi Modestus Lumato,ameiwakilisha Mamlaka hiyo katika Mkutano wa
Jumuiya ya Wadhibiti wa Nishati Afrika Mashariki (EREA), kujadili
masuala mbalimbali ya ushirikiano katika udhibiti wa sekta ya Nishati .Mkutano huo umefanyika jana, Desemba 13,2022 jijini Kigali nchini Rwanda.
Mkutano
huo umehudhuriwa na wanachama wake ambao ni taasisi za udhibiti kutoka
nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni AREEN ya Burundi, EPRA ya
Kenya, ERA ya Uganda, PURA ya Tanzania, ZURA ya Zanzibar, ARE ya DRC,
RURA ya Rwanda na EWURA ya Tanzania.
Kikao
kazi hicho kitafuatiwa na Mkutano wa Bodi Huru ya Kiudhibiti (IRB -
Independent Regulatory Board) inayosimamia Muungano wa Taasisi za
Nishati za Afrika Mashariki (East African Power Pool ) kuanzia tarehe 15
Desemba 2022 jijini Kigali ambapo Djibouti , Ethiopia na Misri pia
zitashiriki.
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Mhandisi Modestus Lumato,(mbele kushoto), akishiriki Mkutano wa Jumuiya ya Wadhibiti wa Nishati Afrika Mashariki (EREA) unaojadili masuala mbalimbali ya ushirikiano katika udhibiti wa sekta ya Nishati uliofanyika leo Desemba 13,2022 Mjini Kigali, Rwanda.
No comments:
Post a Comment