Lions
Club International wametoa msaada wa dawa zenye thamani TZS 15 Mil kwa
ajili ya matibabu ya watoto wanaogua saratani katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili.
Akizungumza
wakati wa kupokea msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa
Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema serikali imechukuwa nafasi kubwa
kwenye matibabu ya watoto wanaougua saratani kwani matibabu yao ni
gharama na yanachukuwa mda mrefu.
“Tunashukuru
kwa msaada huu pia tunawakaribisha wadau wengine kuja kusaidia
Hospitali yetu ya Taifa kwani uhitaji ni mkubwa kulingana na idadi ya
wagonjwa”amesema Prof. Janabi.
Kwa
upande wake, Bw. Mustansir Gulamhussein ( District Governor) amesema
wameguswa kuja kutoa msaada wa dawa kwa watoto wenye saratani ikiwa ni
malengo yao ambayo wamejiwekea.
“Suala
la afya ni kipaumbele chetu sisi kama Lions Club International watoto
ndio taifa la kesho hivyo ni jukumu letu kuwasaidia” amesema Bw.
Mustansir.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)





No comments:
Post a Comment