Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa
kushoto na Katibu Mtendaji wa baraza la usafirishaji Meli (TSC), Sallu
Johnson wa katikati, wakipata maelekezo kutoka kwa Hellen Ignatus
aliyebuni mfumo maalamu wa kuoshea magari kwa muda mfupi na kwa weledi (
automatic car wash system).
Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa
akizungumza wakati wa ufunguzi wa tamasha la Taaluma lijulikanalo kama
Career Fair lililoandaliwa na Chuo hicho kwa lengo la kuwajengea uwezo
wanafunzi katika kukabiliana na soko la ajira nchini.
Baadhi ya wadau na wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha usafirishaji NIT, wakifuatilia hotuba ya Katibu Mtendaji wa baraza la usafirishaji meli (TSC) Sallu Johnson hayupo pichani, wakati wa ufunguzi wa tamasha la Taaluma lijulikanalo kama Career Fair lililoandaliwa na Chuo hicho kwa lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi katika kukabiliana na soko la ajira nchini
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
KATIBU
Mtendaji wa Baraza la Usafirishaji nchini (TSC) Sallu Johnson amekitaka
Chuo cha Usafirishaji nchini (NIT) kuendelea kuboresha mitaala ya
mafunzo vyuoni kwa kushirikiana na wadau wa sekta hiyo ili kuendana na
soko la ajira za wataalamu wa sekta hiyo.
Hayo
ameyabainishwa leo Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Tamasha la
taaluma liitwalo Career Fair lililoandaliwa kwa lengo la kuwajengea
uwezo wanafunzi katika kukabiliana na hali ya soko la ajira nchini.
Amesema
malengo ya kujifunza masuala ya kazi yanasaidia kutimiza malengo ya
uanzishwaji wa chuo hicho kwa kuboresha taaluma za wanafunzi na kuakisi
dira ya maendeleo ya nchi ya kujenga mifumo imara ya sekta ya
usafirishaji.
Ameeleza
kuwa fursa ya kujifunza kwa vitendo inasaidia wanafunzi kuelewa namna
ya kufanya kazi zao vizuri na lengo la kujenga kizazi chenye weledi.
"Naamini
kuwa tukio hilo litakuwa chachu ya ushirikiano baina ya chuo na wadau
wa sekta ya usafirishaji na kufikia soko la ajira kwa kuboresha mitaala
ya mafunzo chuoni na ushirikiano wa wadau," amesema Johnson.
Ametoa
rai kwa wawakilishi kutoka sekta za umma na binafsi kuendelea na
ushirikiano huo kwa sababu jukumu la kujenga wanataaluma waliobobea sio
la chuo pekee.
"Tamasha
hili la taaluma unaendana na juhudi ya kuunganisha taasisi za elimu na
wadau walipo kwenye soko la ajira, wanafunzi watapata fursa ya
kujifunza na kuelewa mabadiliko yaliyopo kwenye soko la ajira duniani na
sekta binafsi imepewa nafasi kubwa ya kuchangia maendeleo hivyo
wanafunzi wanajukumu la kuongeza uelewa huku wakiwa na mkakati wa
kutosha kukabiliana na soko la ajira," amesisitiza.
Kwa
upande wake mkuu wa chuo hicho Profesa Zakaria Mganilwa amesema tamasha
hilo limewakutanisha wadau wa sekta za usafirishaji na wanafunzi wa
chuo hicho ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo pamoja na kupata
uelewa wa soko hali ya soko la ajira nchini.
Profesa Mganilwa amesema kumekuwa na nafasi kati ya wanavyofundisha chuoni na vilivyomo kwenye soko la ajira.
Ameongeza
kuwa katika kutengeneza daraja hilo wameona kuwa na tamasha hilo ili
walimu na wanafunzi wapate fursa ya kujifunza kutoka kwa waajiri ili
kuboresha taaluma zao na kuwajengea uwezo wa kutambua soko la ajira
lilivyo.
"Kuwahamasisha
vijana wetu kujiajiri na kuajiri wengine. Chuo kimebadilika sana kwani
wanaprogramu nyingi shahada za kwanza 15, diploma 25 na jumla ya
wanafunzi 14,000," amesema Profesa Mganilwa.
Pia
amesema chuo kinajivunia kwamba ndoto za waasisi wao zimetimizwa za
kuboresha sekta ya usafirishaji wa maji, reli, anga na kebo na wapo
wanafunzi wa kutosha katika kozi zote.
Aidha
amesema tamasha hilo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika
uboreshaji miundombinu ya usafirishaji ikiwemo ujenzi wa reli, ujenzi wa
bandari pamoja na ujenzi wa meli kwa kuwaandaa wataalamu wazawa
waliobobea katika sekta hiyo.



.jpeg)






No comments:
Post a Comment