NAIBU
Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja amesema Serikali itaunda
Kamati ya kuangalia migogoro ya mipaka na vijiji vinavyozunguka Msitu wa
Hifadhi wa Bonde la Wembere uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Iramba mkoani Singida.
Ameyasema
hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi kuhusu mgogoro wa mipaka
kwenye eneo la ardhioevu katika Kijiji cha Msai na Ujungu mkoani
Singida.
Amesema
Kamati hiyo itaishauri Serikali endapo kuna umuhimu wa kurekebisha
mipaka na kama eneo hilo litafaa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu au
la.
"Kuanzia
leo tunaunda Kamati ambayo itajumuisha wataalam kutoka ngazi ya
Wizara,Mkoa na Wilaya na zoezi hilo litaanza mara moja na itapitia
mipaka kwa kushirikiana na wananchi ili kuainisha mipaka halisi kwa
kuzingatia ramani iliyopo ili kumaliza mgogoro huo," amesisitiza
Masanja.
Mary
Masanja amewataka wananchi hao kuzingatia sheria za kutovamia maeneo ya
hifadhi na kuwa walinzi wa eneo hilo mara tathmini itakapokamilika.
Kuhusu
changamoto ya wafugaji wanaopitisha ng'ombe katikati ya hifadhi kwa
ajili ya kupeleka mifugo yao kunywa maji amesema, Serikali itaangalia
namna iliyo bora ya kutatua changamoto hiyo ili wananchi wasiingiliane
na masuala ya uhifadhi.
Sambamba
na hilo amewataka wananchi waache tabia ya kukata miti hovyo na
kukubaliana na mradi wa upandaji miti ulioletwa na Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi.
Kwa
upande wake Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha na
Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka viongozi wa Kata na vijiji
kushirikiana na Kamati iliyoundwa wakati wa kupitia upya usahihi wa
bikini zilizowekwa..jpeg)
.jpeg)

.jpeg)






No comments:
Post a Comment