MHE. MCHENGERWA: UWEKEZAJI BANDARINI KUONGEZA MAPATO YA SERIKALI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, July 18, 2023

MHE. MCHENGERWA: UWEKEZAJI BANDARINI KUONGEZA MAPATO YA SERIKALI


NA JOHN MAPEPELE 

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kupitia Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Mchengerwa  amefungua  Shina la Ushirika la Umoja wa Vijana wa Ikwiriri wilayani Rufiji na kuwataka  kuwapuuza watu wanaopinga  uwekezaji  unaofanywa  na Serikali katika bandari ya Dar es Salaam.


Mhe. Mchengerwa ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii amesema hayo  mara baada ya  kuzindua rasmi wa Shina  hilo na kupandisha Bendera ya CCM ambapo pia aliwapa kadi za CCM vijana kadhaa waliohama kutoka vyama vya upinzani.



Mhe. Mchengerwa amefafanua  kuwa  mpango wa  uwekezaji unaofanywa na Serikali katika bandari hiyo unakwenda kuingiza  mapato  makubwa ambayo yatasaidia  kusukuma sekta nyingine  ukilinganisha na mapato kidogo  yanayopatikana sasa.

Aidha, amewasihi watu wenye  hoja za msingi  kuziwasilisha  serikalini ili zifanyiwe kazi badala ya  kuwadanganya wananchi kwa tamaa zao za kutaka kushika dola.


Amewataka  vijana  kufanya kazi kwa  bidii ili  kukuza mapato yao na  uchumi wa taifa zima kwa kujumla na kufafanua kuwa hayo yanawezekana endapo  vijana  hawataruhusu amani ya nchi ichezewe  na watu ambao amewaita ni waroho wa madaraka.

“Tusiruhusu watu wachache walipasue taifa hili kwa kusema uongo na kushawishi watu, tunapaswa kuilinda amani hii tuliyoachiwa na baba wa Taifa kwa nguvu zetu zote, uzuri wa Tanzania ni kwa sababu Tanzania ina amani.



Tutahakikisha Tanzania inaendelea kuwa moja” amesisitiza Mhe. Mchengerwa


Amesema hivi  karibuni kumekuwa na watu wachache ambao wanatumia ajenda ya kupinga uwekezaji katika bandari ili waweze  kushika dola jambo ambalo amesema  halikubaliki


Amewataka  kujiunga katika vikundi ili waweze  kujirasimisha na kuweza kukopesheka  kirahisi na  kupata  fedha za maendeleo kwa ajili ya kufanyia uwekezaji katika shughuli mbalimbali za biashara.



Aidha amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya maendeleo hivyo hakuna sababu ya watanzania  kudanganywa  na  watu wasiyoitakia mema Tanzania.

Tukio la uzinduzi wa shina la CCM lilipambwa na wasanii wa wilaya ya Rufiji ambao walitoa burudani ya kukata na baada ya hapo Mhe. Mchengerwa alipita kuzungumza kupokea kero mbalimbali za wananchi katika viunga vya mji wa Ikwiriri.

No comments:

Post a Comment