Naibu Waziri wa maji , Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ameambatana na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Mary Pius Chatanda kwenye Ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi ambapo Ndugu Mary Pius Chatanda amekagua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji huduma ya maji vijiji vya Nandagala A & B uliopo Wilaya ya Ruagwa.
Wakati wa Ziara hiyo, Naibu Waziri wa Maji ameeleza dhamira ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namna anavyotua ndoo wakina mama kwa vitendo kwa utekelezaji miradi mingi ya maji hapa nchini.
Katika Wilaya ya Ruagwa kwa mwaka fedha 2023/24, Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa maji kwa kutumia chanzo cha Mto Nyangao ambapo Mkandarasi wa ujenzi ameshalipwa advance payment na yupo site kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
No comments:
Post a Comment