NA HUSSEIN NDUBIKILE, DAR ES SALAAMA
KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu amesema migogoro ya kifamilia inachangia watoto kuwa katika hali mbaya ya malezi na kuongezeka ukatili dhidi yao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Viongozi wa Dini na Serikali, Dkt. Jingu amesema kwa watoto 335,971, walibainishwa kuishi katika mazingira hatarishi na kufanya kazi mtaani hadi kufikia Machi, 2023.
“Jumla ya watoto 2,185 kati yao wa kiume 1,324 na wa kike 861 waliokuwa wanafanya kazi na kuishi mitaani waliunganishwa na familia zao ili kuwasaidia watoto hao ambapo Serikali imeratibu uanzishwaji wa Makao ya Watoto 333 ya Serikali na Binafsi ambayo yanahifadhi watoto 12,077.” amrsema Dkt. Jingu.
Dkt. Jingu amebainisha kwamba, kufuatia hali hiyo Serikali imeandaa mwongozo unaoelekeza namna bora ya malezi ya watoto na familia kwa kuzingatia mazingira na kusisitiza zaidi wajibu wa wazazi au walezi katika malezi ya watoto na familia.
“Mwongozo huo wa kitaifa unajulikana kama Familia Bora, Taifa Imara: Mwongozo wa Taifa wa Wajibu wa Wazazi na Walezi katika Malezi ya Watoto na Familia wa mwaka 2023 Lengo la lake ni kujengeana uelewa na uzingatiaji wa masuala ya msingi kama Taifa juu ya Wajibu wa Wazazi au Walezi kwenye malezi ya Watoto na Familia” ameongeza Dkt. Jingu.
Akitoa salam za Jumuiya ya Kikristo Tanzania Mwenyekiti mwenza wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Askofu Dkt. Stanley Hotay alisema Maadili kwa sasa yameporomoka hususani kwa upande wa watoto wa kiume.
“Tunawapa majina ya watoto wa mitaani, watoto wale sio yatima wana wazazi ila migogoro ya familia, ugumu wa maisha, matumizi ya dawa za kulevya na vingine vingi tufikiri kuwa kama wazazi wetu wangetulea vibaya leo tungekuwa hapa” amesema Askofu Hotay.
Awali Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Sebastian Kitiku, alisema Kikao hicho kitatoka na Mpango kazi wa Malezi baada ya kukaa na wataalam kutoka pande zote zinazohusika
No comments:
Post a Comment