NA MWANDISHI WETU
WATANZANIA wanatakiwa kuamiani kuwa uongozi wa Dk Samia
Suluhu Hassan auwezi kutenganishwa na wa hayati Dkt. John Magufuli na ndio
sababu inayofanya miradi ya kimakakati kuendelea kutekelezwa kikamilifu.
Mathias Kabadi ambaye ni Mtanzania wa kwanza kuandika kitabu
kuhusu hayati Magufuli, ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kitabu cha pili
ambacho kimetungwa na Prof. Malango Chintheng kutoka Chuo cha Hebron (UHB), Lilongwe nchini Malawi.
“Rais Dkt Samia, ni zao la hayati Dkt. Magufuli hivyo uwezi
kuwatenganisha ndio maana miradi
iliyoanzishwa katika uongozi wake inaendelea kutekelezwa ikiwamo Bwawa la
Mwalimu Nyerere, Standard Gauge Railway (SGR), Fly Overs ya Chang’ombe na hakuna ambao
umesimama na itakamilika.
“Awali mwaka 2020 niliandika kitabu kuhusu hayati Magufuli kinachoitwa 'MJUE DKT. JOHN POMBE MAGUFULI', kuna baadhi
ya watu waliamini ni kutokana na kutoka naye ukanda mmoja au sababu ya ukabira
lakini mwaka huu, ametokea mtu mwingine tena kutoka nje ya nchi ameandika kitabu kingine na leo
tunakizindua,” amesema.
Amesema kuwa Dkt Magufuli ataendelea kuandikwa kutokana uongozi wake kugusa maisha ya watu hususan masikini na aliamini Afrika si masikini kutokana na rasilimali ilizonazo.
Naye mwandishi wa kitabu hicho ambacho ni cha pili kuandika
kuhusu hayati Magufuli na kuzinduliwa jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2023 Prof.
Malango Chinthenga kutoka Chuo cha Hebron nchini Malawi, amesema ametumia muda
wa miaka sita kukusanya taarifa mbalimbali zinazomuhusu, Dkt Magufuli, katika
uongozi wake ambao umeleta chachu na mabadiliko makubwa kwa Bara la Afrika.
Katika kitabu hicho Prof.
Chinthenga anaelezea namna ambavyo Afrika inaweza kuendelea na hatua ambazo
Tanzania ilipiga chini ya uongozi wa Rais hayati John Pombe Magufuli
kiuchumi na kiuongozi.
Kwa mara ya kwanza kitabu hicho kilizinduliwa siku chache
zilizopita jijini Mwanza chini ya usimamizi wa Chuo cha St. Augustine.
Pia mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu hicho, Padri Stephano Musomba ambaye alimwakilisha , Askofu Mkuu wa Katoliki Jimbo Kuu la Dar e Salaam, Thaddeus Ruwa'ichi, amesema kuwa elimu ambayo wamepata watanzania imeathiriwa kutokana na
kutaka kufanyiwa kila kitu.
Amesema kuwa wapo wanaotaka waitwe Prof, Dkt, bila kuufanyia
kazi na kusistiza kinachotakiwa kuangaliwa kwa makini ni mila, malezi kwa
vijana kwa maana wengi wao wanapenda kulelewa hali inayosababisha hata ndoa nyingi
kutodumu.
“Haiwezekani mtu wa
nje anaamua kuandika kitabu kuhusu mtu wetu, sisi tunakwama wapi?, inawezekana
ni kutokana na dharau zetu,” amesema.
Ameongeza kuwa kitabu hicho kinachoitwa Africa Magufuli and Change
(Africa Magufuli na Badiliko) ni vema kisomwe na si kuweka kabatini kwa maana
kinaweza kuleta mabadiliko ya kuishi vema kwani mfumo wa maisha yetu haupo kama
Ulaya, kwa watanzania ni shirikishi.






No comments:
Post a Comment