NA MWANDISHI WETU
BOHARI ya Dawa (MSD) imeingia mkataba na kampuni ya Hainnan International kwa
ajili ya ujenzi wa maghala ya kisasa (WiB)kwa ajili ya uhifadhi wa bidhaaa za
afya, Kanda ya MSD Dodoma.
Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mradi huo, Meneja Miradi wa MSD, Deo
Orauya ameeleza maghala hayo yatakua kitovu (hub) cha uhifadhi na usambazaji wa
bidhaa za afya kwenye Kanda nyingine za MSD hasa zinazohudumia Kanda ya Kati,
Kanda ya Magaharibi, na Nyanda za Juu Kusini.
Amefafanua kutokana na ongezeko la watu na ujenzi vituo vipya vya kutolea
huduma za afya nchini, MSD imejidhatiti kuongeza uwezo wake wa uhifadhi, ili
kuendana na mabadiliko hayo kwa kujenga maghala ya kisasa, ambapo pia utasaidia
uhifadhi na usambazaji wa bidhaa za afya nchini.
Pamoja na hayo amesema makabidhiano ya eneo la ujenzi, yameongozwa na mshauri
mwelekezi Architect Nkini kutoka kampuni ya ABECC, inayomilikiwa na Chuo Kikuu
cha Ardhi -Dar es Salaam.
Ujenzi wa maghala hayo yenye ukubwa wa sqm elfu 5, katika kiwanja
na.92/1&2/Kizota Dodoma, jirani na Ofisi za Kanda za MSD, unatarajiwa
kukamilika ndani ya miezi 10, huku ikiakisiwa huenda ujenzi ukakamilika ndani
ya muda mfupi zaidi ya huo.








No comments:
Post a Comment