TTB YASHIRIKI MAPOKEZI YA WATALII 31 WALIOWAWASILI TANZANIA KWA TRENI YA ROVOS - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, August 20, 2023

TTB YASHIRIKI MAPOKEZI YA WATALII 31 WALIOWAWASILI TANZANIA KWA TRENI YA ROVOS

NA MWANDISHI WETU, DAR  

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki mapokezi ya treni ya kitalii ya Kampuni ya ROVOS iliyowasili nchini Tanzania leo ikiwa na  watalii 31 wakitokea nchini Angola.

Watalii hao wameonyesha kuvutiwa na mandhali ya maeneo ya Tanzania waliyopita wakati wa ujio wao huo wa Dar es Salaam. 

Hayo yamebainishwa na Afisa Utalii Mkuu wa TTB, Alistidia Karaze wakati wa mapokezi ya watalii hao katika kituo cha treni ya TAZARA jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa  kundi hilo limejumuisha watalii kutoka nchi za Ujerumani, Uingereza, Marekani na Dernmark.

Kwa upande wake Meneja wa Treni hiyo, Lyle Ontong amesema safari imechukuwa siku 65 ambapo ilianzia Afrika kusini kuja Tanzania, ikienda nchini Angola na kurudi Tanzania huku ikitarajia kuondoka siku ya kesho Agosti 21, 2023 kurudi Afrika kusini ikiwa na Watalii 67 kutoka Ujerumani ambao wataanzia safari yao katika kituo cha TAZARA jijini Dar nyingine walizopita na kushauri kuwa, Watanzania kupaswa kutunza vivutio hivyo vya asili pomoja na mazingira ya miji  kwa faida ya vizazi vya baadaye na pia kuwavutia watalii wengi zaidi.

"Treni hii kawaida  hufanya safari zake kuanzia nchini Afrika ya Kusini mpaka Tanzania..

Kwa mwaka huu ni safari ya tatu kwa treni hiyo kuleta  watalii nchini. Amesema.

Aidha, Watalii hao 31, wakiwa nchini watatembelea Visiwa vya Zanzibar,  Mji wa Kihistoria wa Bagamoyo, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Hifadhi ya Nyerere.

Ujio huo wa Wageni hao ni miongoni mwa matunda ya Filamu ya Tanzania the Royal Tour iliyoasisiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan inayoendelea kuleta matokeo Chanya na kuvutia watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja kutembelea vivutio vya utalii vya Nchini.


Afisa Utalii Mkuu, Alistidia Karaze akizungumza na Meneja wa Treni ya ROVOS wakati wa Mapokezi wa treni hiyo jijini Dar es Salaam.



        Baadhi ya watalii wakifurahia na kuagana baada ya kuhitimisha safari yao  jijini Dar es Salaam.


Watalii  wakipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kuwasili katika kituo cha TAZARA jijini Dar Es Salaam.

No comments:

Post a Comment