NA ANDREW CHALE, DAR ES SALAAM
Tukio la utoaji wa vyeti limefanyika jana Agosti 26, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo Zungu, amewapongeza Stanbic kwa mafunzo hayo huku akitoa neno kwa wahitimu hao kuzingatia elimu walioipata.
"Biashara sio mtaji, Biashara ni taaluma ambayo Stanbic benki limeona hilo na kuwapatia mafunzo na taaluma kwenu ili kuwakwamua katika umaskini" amesema Zungu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara Stanbic, Fred Max amesema Stanbic Biashara Incubator kusudio sio programu pekee, ni kujitolea kwa hisani na kukuza mafanikio ya miradi ya ujasiriamali.
"Kupitia safu ya rasilimali na huduma za usaidizi wa biashara, tunalenga kuharakisha ukuaji wa kampuni hizi, tukiwapa zana wanazohitaji ili kustawi.
Ikiwemo ujumuishaji wa mtaji, mafunzo na mwongozo, huduma za kawaida,ufikiaji wa mtandao muhimu wa miunganisho na pia kwa kampuni za SME ambayo yanachangia maendeleo ya kimkakati ya nchi yetu." Amesema Max.
Ameongeza kuwa: "Macho yetu yameelekezwa kwenye sekta ambazo zina jukumu muhimu katika ukuaji wa taifa letu kama Kilimo na uzalishaji vifuniko vya ujenzi, kazi za kiraia, na malighafi, Usafiri, Upishi na Hotelier,
Pia kuuza maudhui ya ndani kwa kuimarisha biashara za ndani, kuwezesha kupata kandarasi na kampuni za kimataifa, kuboresha ufikiaji wa uchumi wa ndani na athari kwa kiwango cha kimataifa pamoja na kushughulikia mahitaji ya msururu wa Ugavi
No comments:
Post a Comment