PROF. LIPUMBA: HATUTAKI KURUDISHWA KWENYE SIASA ZA MAPAMBANO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, November 25, 2023

PROF. LIPUMBA: HATUTAKI KURUDISHWA KWENYE SIASA ZA MAPAMBANO


NA MAGENDELA HAMISI

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema akihitaji kurudishwa kwenye siasa za mapambano na wanahitaji kujenga hoja ili nao wawasiliane na wananchi kwa taratibu ambazo zimewekwa na  wanalitaka Jeshi la Polisi kutenda haki hasa wakati wa kuelekea  kwenye uchaguzi za Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.

Prof Ibrahimu Lipumba amebainisha hayo leo Novemba 25 wakati akitoa taarifa za kuvunjwa mkutano wao na baadhi ya viongozi kukamatwa na Jeshi la Polisi kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa hadhara katika viwanja vya Buguruni Sheli Novemba 24, 2023 saa tisa alasiri.

Kiongozi huyo wa CUF Taifa, amefafanua kuwa jana Novemba 24 chama chake kupitia viongozi wa Wilaya ya Ilala waliandaa Mkutano wa adhara na kufuata taratibu zote ikiwemo kulitaarifu Jeshi la Polisi kwa barua na Mtendaji Kata husika, siku saba kabla ya tukio hilo.

Aliongeza kuwa katika kipindi hicho cha maandalizi Jeshi la Polisi halikutoa zuio la mkutano huo,hivyo wanashangazwa kuona viongozi wake wakiwa katika eneo la tukio na yeye akiwa njiani kutaarifiwa kuwa Polisi wamevunja mkutano huo na viongozi saba kukamatwa na kwa sasa nje kwa dhamana.

 “Viongozi wetu wanatakiwa kurejea Polisi Jumatatu Nov 27, 2023 na hatujui watapewa kesi gani, bado vifaa vyetu likiwemo gari la matangazo, laptop, vifaa vya kutangazia na vitu vingine vimezuiwa katika kituo cha Buguruni na tunaendelea kuvifuatilia,” amesema.

Amesema ili kuondoa changamoto hiyo kwa vyama vya siasa ni vema Serikali ikapanga utaratibu wa kutoa mafunzo kwa viongozi wanaohusika kupokea taarifa za mikutano ya hadhara, itakayosadia kuwapa uelewa kuhusu siasa za maridhiano.

Pia viongozi hawa wanatakiwa kujua wakati huu tunaingia katika kipindi cha maridhiano Rais Dkt Samia anatueleza kuwa falsafa yake ni R4, mojawapo ni maridhiano ingawa sasa wapo baadhi ya watu wa chini wanataka kumwangusha jambo ambalo si jema kwa ustawi wa siasa za Tanzania.

“Kama mkutano wa unaofanyika Dar es Salaam unavunjwa je kwa viongozi wa vijijini ambao wanataka kuandaa mikutano hali itakuwaje,” alihoji .

Wakati huo huo Prof. Lipumba ameibanisha kuwa wapo katika mchakato wa kumwandikia barua, Waziri wa Mambo ya Ndani ili aombe radhi kwa kadhia hiyo ambayo chama chake imekipata kwa mkutano wao kuvunjwa na viongozi wao kukamatwa licha kufuata taratibu zote za maandalizi.

No comments:

Post a Comment