Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, akizungumza wakati wa mahafali hayo.
NA MAGENDELA HAMISI
NAIBU Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, ametoa maagizo kwa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo kupanga mkakati chuoni hapo wa kufanya tafiti zitakatoa suruhisho ya changamoto ya mfumo wa ukusanyaji wa kodi nchini.
Chande ametoa maagizo hayo leo Nov 24 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mafahali ya 16 ambayo yamefanyika chuoni hapo ambapo wahitimu 508 walitunukiwa vyeti vyao huku waliofanya vizuri wakipatiwa nafasi za kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) moja kwa moja.
“Miongoni mwa changamoto kubwa ambayo tunakutana nayo ni ukwepaji wa kodi na kutobaini vyanzo rafiki vya ukusanyaji wa mapato, hivyo kwa weredi wenu ninawaomba mfanye tafiti ya kutatua changamoto katika mfumo wa kodi na forodha na kurahisisha ulipaji kodi kwa hiari” amesema.
Pia amesema Serikali inatambua kuwa zipo biashara zinazofanywa mitandaoni, hivyo ni vema huko nako kodi ikakusanywa kikamilifu kwa kutengeneza mfumo rafiki bila kuathiri hizo biashara na wafanyabiashara husika.
Naibu Waziri, Chande ameongeza kuwa kwa sasa dunia imebadilika kila kitu kipo kwenye utandawazi, hivyo amesisitiza uongozi wa chuo hicho katika tafiti watakazofanya kuhakikikisha wanaishauri Serikali namna bora ya kukusanya mapato kupitia bishara mtandao.
Aliongeza kuwa ukusanyaji mapato linahusu wadau wengi wakiwemo watunga sera, watoza kodi na walipa kodi, hivyo TRA inawajibu wa kukisaidia chuo kupanua wigo wa kutoa mafunzo kwa wadau ili taifa lipate wataalamu waadilifu wa kutosha na walipa kodi wazalendo watakaotambua wajibu wao wa kulipa kodi bila shuruti.
“Nawaomba pia mwanzishe kozi fupi kwa ajili ya walipa kodi, kwani tumebaini wengi wao hawana elimu ya kutosha ya ulipaji wa kodi hali inayosababisha kuhamisha jukumu hilo kwa washauri wao ambao nao changamoto yao ni anaweza kuwa mhasibu lakini hana taaluma ya kodi,” amesema.
Naye Mkuu wa chuo hicho Prof, Jairo alisema mikakakati ambayo wanayo ni kuongeza mafunzo kuhusu utozaji wa kodi katika sekta ya maalumu katika nyanja zinazoibuka kama sekta ya madini, mafuta , gesi na taasisi za fedha.
Pia wanaendeleza ushirikiano na taasisi za ndani na nje ya nchi na tayari wamehuisha makubaliano na ushirikiano na shirika la kimataifa la utafiti wa kodi IBFD lenye maskani yake Amsterdam Uhoranzi, pamoja na vyuo vinavyotoa mafunzo ya forodha ulimwerngu.
Aliongeza kuwa baada ya jengo la utawala kufanyiwa upanuzi watalitumia kuanzia elimu ya masafa (Online and Distance) jambo litakalosiadia kutoa mafuzo kwa wakati mmoja kwa wanafunzi wengi bila kufika chuoni hapo.
Pia katika mahafali hayo Kamishna Mkuu wa TRA,Alphayo Kidata alitoa rai kwa Baraza la Chuo kuendeleza usimamizi ili kusaidia kuzalisha wahitimu wenye weledi, uadilifu utakaowawezesha kuongeza tija na ufanisi katika utendaji wa kazi.
“Na katika mahafali haya ya 16, wahitimu wa mwaka huu tumeanza na utaratibu kidogo kwa wale ambao wamenya vizuri zaidi watapata nafasi ya kujiunga na TRA moja kwa moja, “amesema.
No comments:
Post a Comment