magendela@gmail.com
SHIRIKA la Furahika limepokea shilingi milioni 200 kwa ajili ya kuendeleza mradi wa Elimu Bure kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka wa miaka 13 hadi 24 ambao wamekosa fursa ya kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia.
Kwa sasa vijana mbalimbali wanaendelea kusajiliwa kwa ajili ya muhula mpya wa masomo na mwisho wa usajili ni Janauri 28, 2024 na wazazi ama walezi wametakiwa kutumia nafasi ili kutoa fursa kwa vijana wao kupata elimu bure bila malipo.
Kaimu Mkuu Kituo cha Furahika kilichopo Buguruni Malapa Ilala, jijini Dar es Salaam, chenye usajili namba VET/DSM/PR/2021/D169, Dkt. David Msuya amesema: “Vijana tunaowapokea kwa ajili ya masomo ni wale walioshindwa kuendelea na shule kwa kupata alama hafifu katika matokeo ya darasa la saba, kidato cha pili na nne ama kushindwa kulipa ada, hapa tunawakaribisha ili watimeze ndoto zao na kuepuka utegemezi,” amesema Dkt. Msuya.
Ameongeza kuwa kituo hicho kazi yake ni kuwapokea vijana na kuwasaidia kuwapa ujuzi wa fani mbalimbali ikiwemo kozi ya Utalii, Hotel Management, Ushonaji, IT na nyinginezo zitakazowasaidia kupata ajira ama kujiajiri wenyewe na Januari 2024 watarajia kuanza kufundisha mpya ambazo watazitangaza.
Dkt. Msuya ametanabaisha hayo leo Desemba 18, 2023 jijini Dar es Salaam kuwa tangu kuanza kutoa huduma ya masomo kwa kozi mbalimbali kwa vijana, wengi wanapokwenda Field wamekuwa wakipata ajira kutokana na kuonesha ubora na umahiri mkubwa hususan kwa kozi za hotel.
Pia ametoa shukran kwa Mkurugezi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, kwa kuajili wahitimu wa chuo hicho wa masomo ya upishi katika kituo cha reli, Mlandizi jambo ambalo kwa chuo imekuwa ni faraja kubwa kwao.
Amefafanua kuwa chuo hicho kinafanya kazi zake kwa mujibu wa utekelezaji wa miradi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum kupitia Ustawi wa Jamii.
Kutokana na wiki hii kuwa ya kupinga vitendo vya ukatili, Dkt. Msuya ametoa wito kwa Serikali kuangalia namna ya kutunga sheria ya kuwadhibiti baadhi ya wazazi ama walezi wenye tabia ya kutumikisha watoto wakati wa muda wa masomo kwa kutembeza biashara kama mbogamboga, matunda n.k.
“Baadhi ya watoto utawaona wanatembeza biashara wakati wa masomo wenzao wakiwa darasani huo nao ni ukatili na unapaswa kukemewa na kuwachukulia hatua wazazi, walezi wanaokwepa majukumu yao ya kutafuta kipato kwa ajili ya familia badala yake wanawatumia watoto kubeba mzigo huo,” amesema.
Baadhi ya wanafunzi wanaotaka kujiunga na chuo hicho kwa muhula mpya wakisubiri kuhudumiwa.
No comments:
Post a Comment