KAMANDA MULIRO ATAKA TAARIFA UPANDAJI MITI KILA MWEZI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, February 17, 2024

KAMANDA MULIRO ATAKA TAARIFA UPANDAJI MITI KILA MWEZI


NA JESHI LA POLISI, DAR ES SALAAM

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP. Muliro J. Muliro, amezindua kampeni ya upandaji miti katika maeneo yanayomilikiwa na Polisi Jijini Dar es Salaam. 


Uzinduzi huo umefanyika Leo Feb 17, 2024 katika kambi ya Polisi Kijichi ambapo SACP. Muliro amesema baada ya kupanda miti hiyo ametaka kupata taarifa za maendeleo ya ukuaji wa miti hiyo kila mwezi, kama namna ambavyo kumekuwa na ufuatiliaji wa taarifa za uhalifu.


SACP. Muliro amebainisha kuwa miti hiyo itapandwa katika maeneo mbalimbali yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam yanayopatikana Kigamboni, Mabwepande na Mwanagati ikihusisha jumla ya miti 3000.


Kampeni hiyo kitaifa ilizinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, Februari 7, 2024 Jijini Dodoma ikiwa na lengo la kupanda miti katika maeneo yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi Nchini.






No comments:

Post a Comment