Steve Nyerere (wa pili kulia)ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao akizungumza na waandishi wa Habari.
NA MAGENDELA HAMISI
TAASISI ya Mama
Ongea na Mwanao, imewataka wanasiasa kuacha kufanya siasa za matusi na
kumkashifu Rais, Samia Suluhu Hassani.
Pia amelitaka
Jeshi la Polisi kutokaa kimya kwa wanasiasa wanaomtukana Rais mitandaoni kwani wanatakiwa
kukamatwa na kuhojiwa na wakipatikana na hatia wapandishwe kizimbani wakajibu
tuhuma zao.
Hayo yamezungumza leo Machi 11, 2024 jijini
Dar es Salaam na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Steve Nyerere na kusisitiza hawezi
kukaa kimya kuona Rais Samia, akitukanwa na baadhi ya wanasiasa wanaofanya
siasa chafu.
Pia ameshangazwa na kuona kijana ambaye
ametusi Rais akiwa bado hajakamatwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama huku chama
chake cha siasa kikiwa tayari kimefukuza uanachama.
“Huyu mtu nguvu
ya kumtukana rais anaitoa wapi na yuko nyuma ya nani na kwa nini hadi leo hajakamatwa,”
alihoji Steve Nyerere.
Ameongeza kuwa
ifike wakati baadhi ya wanasaisa wakachunga kauli zao kabla ya kusema ili
kujenga amani na utulivu nchini.
“Tunalaani
kitendo hicho kwa mtu huyo kumtukana Rais mitandaoni na tunatoa wito kwa
wanasiasa kufanya siasa za hoja bila matusi ambayo hayana afya kwenye siasa,”
amesema.
Pia amewataka
watu ambao wapo karibu na Mama (Rais) kuhakikisha wanakuwa imara katika
kuwadhibiti na kutokaa kimya kwa wanasiasa wanaomtukana rais mtandaoni.
“Mlio karibu na
Mama, msikae kimya mama anapotukanwa, mnatakiwa kujibu, hakuna mtu anaweza
kukaa kimya huku mama yake anatukanwa, haiwekani,” amesema.
Wakati huo huo,
Steve Nyerere ametoa wito kwa vijana kutumia vema mitandao kwa ajili ya
kujiongezea kipato na si kufanya mambo ambayo yatawafanya kuwa masikini.





No comments:
Post a Comment