MIAKA MITATU YA RAIS DKT. SAMIA TANZANIA YANG’ARA KIMATAIFA KIDIPLOMASIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, March 20, 2024

MIAKA MITATU YA RAIS DKT. SAMIA TANZANIA YANG’ARA KIMATAIFA KIDIPLOMASIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, (Wa kwanza kulia) Januari Makamba akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichani leo Machi 20, 2024 jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo yamefanikisha Tanzania kung'ara kimataifa katika nyanja ya diplomasia.

NA MAGENDELA HAMISI

WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeweka wazi kuwa miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani, Tanzania imefanikiwa kung’ara katika nyanja mbalimbali duniani mojawapo ikiwa ya Kidiplomasia.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam Machi 20, 2024 na Waziri wenye dhamana ya Wizara hiyo , Januari Makamba wakati akizungumza na waandishi wa Habari na kufafanua kuwa takwimu za mtaji katika uwekezaji kwa mwaka 2020 ulikuwa ni dola billion 1.03.

Ameongeza kuwa mwaka 2023 takwimu zinaonesha mtaji kutoka kwa wawekezaji umefikia bilioni 5.6 hali ambayo ni ya kupongezwa kulingana na mafanikio hayo ya kujivunia katika kipindi cha miaka mitatu cha Rais Samia.

Makamba amesema kutokana na kupata mafanikio hayo, yamesababisha hata baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka nje ya nchi kuja nchini kuomba ushauri kwa Rais Samia ili nao wakajipange na wapige hatua kama ilivyo Tanzania.

“Hii inadhihirisha namna Rais wetu Dkt. Samia anavyokubalika kimataifa na ni jambo la kujivunia na kupitia yeye taifa letu limekuwa likipata mafanikio kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati kupitia mikopo ya masharti nafuu.

"Mafanikio haya yanatokea kutokana na ushawizi mzuri alionao Rais wetu katika nyanja ya kimataifa na kusababisha wageni wengi kuja nchini kwa masuala mbalimbali ikiwemo kujifunza hivyo tuna kila sababu ya kujivunia kuwa na kiongozi mwenye upekee," amasema.

Katika kujiweka sawa katika nyanja ya kidemokrasia, Wizara hiyo pia imezindua Kamati Maalumu itakayokuwa na jukumu la kusimamia na kushughulikia Chuo Cha Uhusiano wa Kimataifa Diplomasia Cha Salim Ahmed Salim.

Kwa mujibu wa Waziri Makamba, kamati ambayo imeteuliwa ikiwa na wajumbe wake saba wabobezi na wenye sifa stahiki katika masuala ya diplomasia za kimataifa huku pia wakiwa wametumikia taifa katika nyadhifa kadhaa na kuwa na uzoefu wa kutosha.

 Amesema kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake, Balozi Khamis Kagasheki, makamu ni Balozi Ramadhani Dau, wajumbe ni Prof. Masilina Chinoriga, Dkt Salim Ali, Dkt Singo,Dkt Shule, Dkt Sanga na Ashumta Muna.

Aidha Waziri Makamba amesema kazi za kamati hiyo ni kupendekeza muundo wa kisheria wa uongozi wa kituo aina ya mafunzo na mitaala ya chuo, pia itakuwa na uwezo wa kubuni fikra za aina ya uongozi wa chuo.

Pia amesema itakuwa na uwezo wa kupendekeza muundo wa uombaji wa ajira kwa watumishi na wafanyakazi wa chuo na itakuwa na kazi ya kujua ni namna gani chuo kitaweza kujiendesha na kubuni njia za kujipatia fedha za kujiendesha na kutoa maoni na ushauri kwa Wizara kwa masuala yenye tija kwa Chuo.

Ameongeza kuwa Chuo hicho ni moja ya chuo kikongwe barani Afrika kilichojizolea sifa lukuki kutokana kuzalisha viongozi wengi wa ndani na nje ya nchi.

Pia Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Kagasheki amemshukuru, Waziri Makamba na kamati yake kwa uteuzi wake na imani kubwa waliyonayo kwake.

 

No comments:

Post a Comment