Kamishna wa Uhifadhi TAWA, Mabula Nyanda akizungumza leo Machi 18, 2024 akielezea mafanikio yao kwa kipindi cha miaka mitatu.
NA MAGENDELA HAMISI
MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA)
katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan, inajivunia kutekeleza
majukumu yao kiufasaha ikiwemo kuongeza watalii baada ya kuwezeshwa kifedha.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 18,
2024 katika mkutano na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari
nchini, Kamishna wa Uhifadhi TAWA, Mabula Nyanda amesema kwa katika kipindi
hicho wamefanikiwa kuongeza idadi ya watalii.
“Mwaka 2020/21 tulianza na watalii 37, 684 na
mwaka 2022/23 tumepata watalii 166, 964 kwa mwaka huu hadi kufikia Feb
tumefanikiwa kuingiza watalii 116, 529 na tutakapomaliza mwaka tunaratajia
kufikia malengo makubwa zaidi, amesema.
“Na yote hayo yamechangiwa kwa asilimia kubwa
na Rais wetu, Dkt Samia Suluhu Hassan kutuwezesha kifedha na filamu ya Rolay
Tour kufanya kimataifa jambo ambalo limesadia kuitangaza Tanzania na watalii
kumiminika kwa wingi, amesema
Amesema kuwa tofauti na watalii kuja nchini,
pia meli kubwa za kitalii mwaka 2020/21 ziliingia nne na mwaka 2023/ 24
zimefanikiwa kuingia meli nane jambo ambalo ni mafanikio makubwa kwa TAWA na
Serikali kwa ujumla.
Ameongeza kuwa mafanikio mengine baada ya kuwezeshwa
na Rais Dkt Samia katika kipindi cha miaka mitatu tangu aingie madarakani ni
kuhimalisha ulinzi wa rasilimali, wanyamapori na malikale.
Amefafanua kuwa kwa kupindi hicho cha miaka
mitatu ya Rais Samia, wamefanikiwa kupunguza ujangili wa tembo kwa asilimia 83,
ambapo kwa mwaka 2021/22 kuwa na mizoga sita hadi kufikia mizoga mitatu kwa
mwaka 2023/24.
Ameongeza kuwa yote hayo yamesababishwa na
kupata vitendea kazi vinavyosaidia kuhimilisha mtandao wa kitelejinsia wa
kupata taarifa mbalimbali ujangili inayozeshwa ufungwaji wa visukuma mawimbi
kwa tembo.
Pia TAWA katika kipindi cha miaka mitatu,
wanajivunia kupunguza migogoro ya mipaka na wananchi katika mapori ya Akiba
saba na moja likiwa katika hatua za mwisho kukamilika ili kuweka hali shwari
kwenye jamii.
Kamishna Mabula amesema migogoro ambayo tayari
wameimaliza ni katika mapori saba ambayo ni Mkungunero, Swagaswaga, Igombe,
Wamimbiki, Mpanga Kipengere, Selous na Liparamba huku Kilombero likiwa katika
hatua za mwisho kumalizia mgogoro.
Katika utatuzi wa migogoro kwenye eneo la ekari
103, 544.48 ambalo limemegwa kutoka hifadhi na kuwapa wananchi kwa ajili ya
shughuli za kiuchumi, serikaloi kupitia TAWA, inaendelea kulipa fidia kaya 45
zilizo katika pori la Akiba Mkungunero.
Ameongeza kuwa anaamini hali itaendelea kuwa
tulivu kutokana na kushirikiana na jamii vema na kuchangia miradi ya maendeleo
katika maeneo husika ikiwemo ujenzi wa masoko, madarasa.
Katika hilo Kamishna Mabula amesema katika
kipindi cha mwaka 2021/24, wamechangia katika miradi ya jamii shilingi milioni
193 ambapo kwenye ujenzi wa soko la samaki katika mji wa Ifakara Kilombero
wametumia mil 66.
Pia wamenunua mashine mbili za kusaga mkoani
Mara na kuchangia mil 10 katika ujenzi wa Zahanati na vyumba vya madarasa Mwibara,
ikiwemo mil 20 katika ujenzi wa Zahanati ya Bungo ya wilayani Korogwe mkoani
Tanga.
Pia kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa, ofisi
za walimu na ununuzi wa madawati katika Shule ya Msingi Usinge iliyoko Kaliua
mkoani Tabora wametoa sh. mil 50 na
madawati 100 wameyatoa wilayani Bunda.
Katika
mafanuikio yote haya ambayo tumepata kwa kweli tunamshukuru Rais Samia kwa
kutuwezesha, bila yeye tungekuwa na wakati mgumu kufikia hapo, pia katika
kipindo hicho tumefanikiwa kununua magari 60, meli za doria tisa na mashine ya
uchimbaji visima vya maji ambayo yanasaidia kwa ajili matumizi ya wafanyakazi
wetu na raia kwa ujumla, tunamshukuru sana Rais Samia., amesema







No comments:
Post a Comment