DC MALISA KUUNDA KAMATI KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI ENEO LA CHUO CHA KILIMO UYOLE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, April 10, 2024

DC MALISA KUUNDA KAMATI KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI ENEO LA CHUO CHA KILIMO UYOLE

                                                 Mkuu wa  wilaya ya Mbeya, Beno Malisa.

NA MWANDISHI WETU, MBEYA

SERIKALI imeanza mchakato wa kumaliza mgogoro wa ardhi unaoendelea kati ya viongozi wa kimila (Machifu) na Taasisi ya Utafiti ya Kilimo (TARI) katika  eneo la chuo cha kilimo Uyole Jijini Mbeya. 

 Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amefikia uamuzi  huo baada ya kukutana na pande zote mbili,  Machifu na  TARI na kusikiliza hoja za pande hizo ambapo machifu wanadai eneo la  hekari  nane walilotengewa  sio eneo sahihi huku wakidai eneo lenye makaburi ya viongozi wao wa kimila waliofariki miaka kadhaa iliyopita ndio eneo sahihi wanalopaswa kukabidhiwa.

Kwa upande wa kituo cha utafiti wa kilimo TARI wanadai kuwa eneo walilowapatia machifu ni eneo sahihi ambalo linawatosha kufanya shughuli zao za kimila ambapo gharama zimetumika kuweka uzio kwa ajili ya kulitambua eneo hilo na kwamba halitotumika kwa ajili ya shughuli za kilimo. 

Aidha Malisa ametaka kuundwa kwa kamati itakayojumuisha baadhi ya watu kutoka upande wa  machifu na upande wa TARI kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ili  kulipatia ufumbuzi suala hilo haraka iwezekanavyo.

Pia Malisa, amezitaka pande zote mbili kuwa watulivu katika kipndi hiki ambacho   ya mgogoro huo unatafutiwa ufumbuzi  na kusimamisha shughuli za kimila na kilimo katika eneo hilo mpaka pale ambapo majibu yake yatapatikana siku za hivi karibuni.







No comments:

Post a Comment