NA MWANDISHI WETU, NJOMBE
APRIL 9, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Njombe imefunguliwa kesi ya jinai dhidi ya Lavenda Meshack Nyagori, kwa kosa la Kuomba na Kupokea Rushwa kinyume na Kifungu cha 15 (1)(a) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (cap 329 Re 2022).
Mshtakiwa akiwa Mtendaji wa Kata ya Ninga, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, aliomba rushwa kiasi cha shilingi 120,000 kutoka kwa Bw Joel Daniel Kuyava na kupokea kiasi cha shilingi 100,000 ili amsaidie kutatua mgogoro wa kifamilia ya mwanae Samson Joel Kuyava na mkewe Atira Lutumo.
Akisomewa mashtaka hayo mbele ya Mhe. Romanus Mlowe - Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Njombe, mshtakiwa alikana makosa yote.
Mshtakiwa alipewa dhamana na ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na hivyo yupo ndani na shauri limepangwa kusikilizwa tena Aprili 22, 2024.
No comments:
Post a Comment