MWANDISHI WETU, KATAVI
APRIL12, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Tanganyika, mbele ya Mhe. Sydney Nindi, Hakimu Mfawidhi, imefunguliwa kesi ya Jinai namba CC. 9586/2024 ya Jamhuri dhidi ya NTUNGA SAHANI KUWASANYA (Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagunga Kata ya Kasekese, Wilaya ya Tanganyika, Mkoani Katavi.)
Ntunga anashtakiwa kwa kupokea hongo ya Sh. 320,000 kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022.
Akisoma hati ya Mashtaka, Mwendeaha Mashtaka wa TAKUKURU Bi. Vailet Achimpota amesema, Mshtakiwa huyo kwa tarehe tofauti kati ha Juni 1, 2023 hadi Julai 30, 2023 alipokea hongo hiyo kutoka kwa Wanakijiji 16 wa Kijiji cha Kagunga, Kata ya Kasekese, ili awagawie mashamba katika maeneo ya hifadhi ya Msitu wa Kalaba uliopo Wilaya ya Tanganyika.
Mshtakiwa amekiri kosa na mahakama imemhukumu kulipa faini ya Shilingi 500,000/= au kifungo cha miaka mitatu jela.
Mshtakiwa amepelekwa gerezani baada ya kushindwa kulipa faini.
No comments:
Post a Comment