Mkurugenzi wa TBS, Athuman Ngenya
NA MAGENDELA HAMISI
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu, imeweka wa kutenga kila mwaka shilingi milioni 250 kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo kupata leseni za alama za ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) bila malipo yoyote.
Kutoka na mchakato huo kufanyika kwa wajasiliamali wadogo, kwa kipindi hicho cha miaka mitatu, TBS wamefanikiwa kutoa leseni 2, 106 zinawasaidia kufanya shughuli zao vizuri kuanzia uwaandaji hadi kuingiza sokoni .
Leseni hizo zimewasaidia wajasiliamali hao hao kufungua milango ya kibiashara hadi nje ya nchi kutokana na viwango kukubalika kimataifa kutokana na TBS kuwa miongoni mwa wapangaji wa viwango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo Aprili 15, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa TBS, Athuman Ngenya wakati akizungumza na wahariri pamoja na waandishi wa habari ambapo alitoa taarifa ya utekelezaji na mafanikio ya shirika hilo kwa kipindi cha miaka mitatu.
“Natoa wito kwa wajasilimali wadogo waje kwa wingi kwa maana Rais wetu mpendwa anatoa fedha kila mwaka kwa ajili ya kuwawezesha kupata leseni hizo ili watumize malengo yao kuanzia utayarisha wa bidhaa, kiwanda hadi zinapoingia sokoni kote tunafanya ukaguzi na baada ya kulidhika tunatoa leseni bure bila malipo yoyote kikubwa akidhi vigezo,”amesema.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, wamefanikiwa kusogeza huduma kwa wananchi kwa kuwa na kanda saba zitakazohudumia mikoa ya kimkakati jambo litakalosaidia kupunguza gharama za kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo leseni.
Ameongeza kuwa kwa sasa wanakamilisha ujenzi wa ofisi ya Kanda ya Kati Dodoma itakayokuwa ikihudumia mikoa ya Singida, Dodoma Tabora na baadaye wataanza ujenzi wa ofisi nyingine ya Kanda ya Ziwa na kufuatia Kanda ya Kaskazini, Magharibi, Kusini, Nyanda za Juu Kusini na nyingnezo.
No comments:
Post a Comment