Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendelea ya Makazi, Jerry Silaa akizungumza.
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendelea ya Makazi, Jerry Silaa amewataka watumishi wa ardhi nchini, kuwa waadilifu na hofu ya Mungu kwa kutenda haki wakati wanaposuluhisha migogoro ya ardhi.
Silaa ameyasema hayo mapema leo Aprili 15, 2024, wakati akifungua kliniki ya ardhi Mkoa wa Mbeya itakayofanyika hadi Aprili 17, 2024, Jijini hapa. Amewakumbusha watumishi wa Ardhi kutenda haki kwa wananchi na kuwa na hofu ya Mungu, kwani kushindwa kutatua jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wao ni kumkosea Mungu.
Aidha, Silaa ameendelea kusisitiza kufanya kazi kwa kumsaidia Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini pia kufanya kazi kwa ajili ya wananchi katika upande wa ardhi ili kupunguza kero na migogoro isiyokuwa na ulazima katika jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amempongeza,Waziri Slaa kwa kuitumikia vyema sekta ya ardhi kwa kutatua migogoro mbalimbali nchini ikiwa ni moja ya jitihada za kumsaidia Mhe. Rais kwa vitendo.
Katika Kliniki hiyo ya Ardhi inayofanyika katika ukumbi wa Mkapa, wakazi wa Mkoa wa Mbeya watapata huduma ya kusikilizwa na kutatuliwa changamoto mbalimbali zinazohusu ardhi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.
No comments:
Post a Comment