NA MWANDISHI WETU
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubery Ally Maulid amezindua rasmi Shule ya Sekondari ya Ubungo NHC, iliyopo mkoani Dar es Salaam.
Shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa Ubungo mkoani Dar es Salaam, imegharimu kiasi cha takribani sh bilioni moja imechukuwa wanafunzi 194 kati ya 150 iliyopangiwa.
Katika uzinduzi huo, Maulid amesema ni shughuli iliyopangwa kufanyika katika kipindi cha kuadhimisha miaka 60 ya muungano.
Amesema katika miaka 60 ya muungano serikali imewezesha kupatikana kwa miundombinu bora ya elimu, na kwamba uzinduzi wa shule hiyo ni ushahidi tosha wa mafanikio nchini.
Ametaja baadhi ya faida za muungano kuwa ni mshikamano, ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na wanafunzi kupata elimu bila ubaguzi.
Awali Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Ubungo NHC, Rahabu Nkoo amesema shule hiyo imefunguliwa Januari nane, mwaka huu.
Amesema changamoto wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa uzio kwa kuwa ipo eneo la makazi ya watu.
Amesema awamu ya kwanza ya ujenzi umekamilika kwa asilimia 100, na kwamba ujenzi huo una uwezo wa kubeba sakafu tatu.
No comments:
Post a Comment