TABORA UNITED WAKO FITI KUSAKA POINTI TATU NYUMBANI DHIDI YA KAGERA SUGAR - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, April 16, 2024

TABORA UNITED WAKO FITI KUSAKA POINTI TATU NYUMBANI DHIDI YA KAGERA SUGAR




NA MWANDISHI WETU, TABORA

KIKOSI cha Timu ya Soka ya Tabora United, kesho kitashuka katika Uwanja wa nyumbani wa Ally Hassan Mwinyi, kusaka alama tatu dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.


Kocha Mkuu Denis Goavec wa Tabora United, mapema leo imekamilisha maandalizi yake kwa ajili ya mtanange huo utakaopigwa saa 10:00 jioni  na kutanabaisha kuwa wachezaji wote wapo vizuri na lengo likiwa moja tu kusaka alama tatu.

Nyuki hao wa Tabora, wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kugawana alama katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, uliopigwa kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

“Tunakwenda kwenye mchezo wetu wa kesho, tukifahamu kabisa tunakutana na timu nzuri, yenye wachezaji na benchi la ufundi lenye ubora, tumeifuatilia Kagera Sugar wamekuwa na matokeo mazuri na hata kwenye msimamo pia wapo vizuri,  ila kama Nyuki wa Tabora tutakwenda kupambana.

Kabla ya mchezo huo Nyuki wa Tabora, walitoka sare dhidi ya JKT Tanzania hivyo katika mtanange wa kesho kwa mujibu wa Ofisa Habari wao Christina Mwagala ametamba kwamba wamejidhatiti ili kupata alama tatu dhidi ya Kagera Sugar.


Tabora United inashuka dimbani hiyo kesho ikiwa imejikusanyia alama 22 baada ya kucheza michezo 22 ikiwa na wastani wa kupata alama moja kwa kila mchezo hivyo inahitaji kushinda dhidi ya Kagera ili kusalia kwenye nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi.


No comments:

Post a Comment