TMDA YAONDOA SOKONI DAWA DUNI YA MAJI 'BENYLIN PEDIATRICS SYRUP' TOLEO NAMBA 329304 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, April 15, 2024

TMDA YAONDOA SOKONI DAWA DUNI YA MAJI 'BENYLIN PEDIATRICS SYRUP' TOLEO NAMBA 329304

N

NA ANDREW CHALE 

MAMLAKA ya Dawa na vifaa tiba nchini (TMDA) imetoa taarifa kwa Umma kuondolewa (recall) kutoka katika soko kwa dawa duni aina ya 'Benylin Pediatrics Syrup' toleo namba 329304 ilitengenezwa na 

kiwanda cha Johnson & Johnson (Pvt),cha mji wa Capetown, Afrika ya Kusini.


Katika taarifa hiyo iliyotolewa na kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma , na kusainiwa na Mkurugenzi mkuu wa TMDA, Adam Fimbo imebainisha kuwa:


"TMDA inapenda kuutaarifu umma kuwa imeona taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii hususani makundi sogozi ya 'Whatsapp' kuhusu uamuzi wa Mamlaka za Udhibiti wa Dawa (National Medicines Regulatory Authorities) za nchi kadhaa barani Afrika kuzuia matumizi na kuondoa (recall) katika masoko yao kwa dawa duni  hiyo ya maji ambayo muda wake wa matumizi unaisha mwezi Aprili,2024.  


“Dawa hii ya maji kwa kawaida hutumika kuleta nafuu kwa watoto wenye umri kati ya miaka miwili (2) hadi miaka 12 wanapopata dalili au magonjwa yanayotokana na hali ya mzio (allergic conditions) kama vile kukohoa na mafua yanayosababisha homa.


Aidha, Kufuatia kuwepo kwa taarifa hiyo, TMDA imeanza mara moja kufanya uchunguzi wa dawa husika pamoja na kufuatilia taarifa hii kupitia mifumo yake ya udhibiti wa dawa zinapoingia, kutunzwa, kusambazwa na kutumika nchini ambapo taarifa itatolewa mara moja matokeo ya uchunguzi na ufuatiliaji utakapokamilika.


"Imeeleza taarifa hiyo.


TMDA imeongeza kuwa: "Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa toleo hilo la dawa hiyo liliingizwa nchini Aprili mwaka 2022,


Ufuatiliaji kwa mwingizaji wa dawa hiyo nchini umebainisha kuwa hakuna tena dawa hiyo katika ghala lake. 


TMDA inaendelea kufuatilia ubora wa matoleo mengine ya dawa hii na hivyo inawaelekeza wananchi kuendelea kutoa taarifa katika ofisi za TMDA nchini ikiwa watabaini uwepo wa toleo hilo (329304) katika soko letu ili kuweza kuzuia madhara yanayoweza kusababishwa na utumiaji wa dawa hizo.




No comments:

Post a Comment