NA MAGENDELA HAMISI
BANK ya TCB na Kampuni ya Bima "Metro Life Assurance" wa wamezindua na kuingia makubaliano ya kutoa huduma ya bima watoto ili waweze kuendelea na masomo baada ya wazazi ama wategemezi wao kufariki Dunia.
Akizungumza na waandishi w habari Leo Machi 17, 2024 Meneja wa TCB, Francis Kaaya amesema huduma hiyo inaitwa ADABIMA ambayo ni mahusus kwaajili ya kutimiza ndoto za watoto kuendelea na masomo baada ya wategemezi wao kufariki Dunia na kuachwa wakiwa njia panda hitimisha elimu yao.
kuwalipia ada wmbao wazazi ama wategemezi wao wamefariki ayoitwa ia makubaliano na ... kwa ajili ya kutoa bima ya kuendeleza jukumu la kuwasomesha watoto pindi wazazi ama wategemezi wao wanapofariki Dunia.
"Kupitia ADABIMA ndoto za watoto kuendelea naasomo hazitafifia baada ya wazazi au wategemezi watafariki na kuwaacha wakiwa bado wansoma,"amesema.
Ameongeza kuwa ikiwa mzazi ama mlezi amewakatia bima hiyo watoto wake TCB na Metro Life Assurance watabeba jukumu la kuendelea kuwasoma hadi watakapohitimu masomo yao.
Amesisitiza kuwa hata mtoto akiwa kiwango chochote elimu atasomeshwa hadi amalize masomo yake na kutimiza malengo yake katika nyanja ya elimu na kufuraia maisha.
Ameongeza kuwa bima hiyo inakwenda kumaliza ama kuondoa changamoto ya watoto kubaki njia panda ya kuendelea na elimu baada ya wategemezi wao kufariki.
Amesema kuwa hata mwanafunzi akiwa mwaka wakwanza katika Chuo chochote wao wataendelea kumsomesha hadi amalize masomo yake pia atapewa fedha ya matumizi shilingi milioni moja.
Amefafanua kuwa ADABIMA ipo katika makundi kadhaa ambapo kama mzazi yupo katika makundi atalipia asilimia sita ya ada ya mtoto wake na akiwa yuko pekee atalipia asilimia tano ya ada ya shule ya mtoto wake.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Metro Assurance, Amani Boma, amesema kuwa wameamua kuungana na TCB kutoa huduma hiyo kutoka na kuwa na matawi nchi nzima hali ambayo otasaidia kuwafikia wateja wengi Kwa kipindi kifupi.
"Hii ni bima inayokuja kusaidia kifedha mtoto aweze kulipa hadi atakapomaliza shule baada ya wazazi wake kufariki na ni vema wazazi wengi wakajitokeza kukata ili vijana waweze kutimiza ndoto zao ikiwa wao wataondoka Duniani, amesema
No comments:
Post a Comment