(PICHA KWA HISANI YA MTANDAO)
NA MAGENDELA HAMISI
JUMUIYA ya Waandishi
wa Habari wa Mtandaoni (JUMIKITA) imepanga kuwakutanisha wana mahudhui hayo na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kwa lengo la kujadili
mapinduzi ya tasnia hiyo kupitia mitandao ya kijamii
Hayo yamebainishwa leo
Mei 18, 2024 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa JUMIKITA, Shabani Matwebe na
kufafanua kuwa waandishi zaidi ya 800 wa mtandaoni watakutana na Waziri Mkuu
Majaliwa Jumatatu katika ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
“Jumikita tunaona
kwamba kuna haja ya kuzungumza na wadau mbalimbali wa mitandao ya kijamii na
kujadili kwa pamoja tukiwa na Waziri Mkuu mapinduzi yaliyopo katika tasnia ya
habari na utangazaji kupitia mitandao ya kijamii na changamoto zilizopo ili
kupata njia ya sahii ya kufikia mafanikio,” amesema.
Ameongeza kuwa mkutano
huo utawajumuisha waandishi kutoka kona zote za Tanzania kupitia kandao zao, watu
maarufu na Shirikisho la Serikali ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO)
ikujumuisha wanafunzi ambao wamo katika mahudhui ya habari mtandaoni.
Ameweka wazi kuwa
katika mkutano huo utaambana na kuadhimisha miaka mitatu ya JUMIKITA itakayotoa
fursa ya kuangalia changamoto zilizoko na kuzitatua jambo litakalosaidia
kufikia mafanikio yanayohitajika kupitia tasnia hiyo.
Ameongeza
kuwa baadhi ya mambo machache watakayowasilisha kwa Waziri Mkuu, Majaliwa ni
namna wanavyohitaji kupewa nafasi katika mihaliko katika kuchukua habari kwenye
taasisi mbalimbali nchini kama inavyofanyika katika vyombo visivyokuwa vya
mitandaoni.
No comments:
Post a Comment