BRELA KUANZA KUTUMIA MIFUMO MIPYA YA USAJILI JUMATATU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, June 20, 2024

BRELA KUANZA KUTUMIA MIFUMO MIPYA YA USAJILI JUMATATU

 


NA MAGENDELA HAMISI, MOROGORO

WAKALA wa Usajili wa Leseni za Biashara (BRELA), wamesema kuwa kuanzia Jumatatu, Juni 24, 2024 wanatarajia kuanza kutumia mifumo miwili mipya ya kimtandao katika shughuli zake mbalimbali ikiwemo ya usajili.

Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu kutoka BRELA, Loy Mhando amesema hayo mkoani Morogoro katika semina inayoendelea kwa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam na kufafanua kuwa mifumo hiyo ni maarufu ambayo ni ‘Oline Registration System na Tanzania Business Portal"

Ameongeza kuwa Online Registration System ndio itakayotumika kusajili kampuni na Majina ya Biashara, leseni za viwanda pia ndio mfumo unaotumika kwa alama za biashara na huduma pamoja na Hataza, hivyo kwa anayehitaji kulinda alama yake atawasilisha maombi kupitia mfumo huo wa usajili kwa njia ya mtandao (ORS).

“Muombaji anapoomba lazima awasilishe anataka ulinzi katika daraja lipi, kuna daraja la Alama za Biashara na Huduma ambazo zipo 45 na zimewekwa makundi kulingana na bidhaa zinazofanana, mfano ukitaka kusajili maji utasema daraja 32 ambazo zinahusiana na maji na vinywaji laini.

Hivyo daraja kuanzia 1 hadi 34 zinahusika na bidhaa, daraja 35 hadi 45 zinahusika na huduma kwa hiyo maombi yanapowasilishwa kama ni Mtanzania awe na namba ya Nida, raia wa kigeni hawezi kuomba moja kwa moja lazima atumie wakala wa ndani.

Pia ameongeza kuwa mwombaji anaweza kuwa mtu binafasi au kampuni na kusisitiza kuwa jina la biashara haliwezi kuomba ulinzi wa alama za biashara na huduma kwa sababu haina utu kisheria, Kampuni ina utu kisheria hivyo inaweza kuomba alama ya biashara na huduma.

Ameongeza kuwa ada za usajili wa alama zipo katika makundi tofauti na hazilipwi kwa wakati mmoja huku akibainisha kuwa ada ya maombi ni shilingi 50, 000, pia kabla ya ada haijatangazwa ni takwa la kisheria kwamba kabla haijasaliwa lazima itangazwe ili kutoa nafasi kwa wapingamizi.

 

 

No comments:

Post a Comment