BRELA YATAHADHARISHA WAFANYABIASHARA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, June 20, 2024

BRELA YATAHADHARISHA WAFANYABIASHARA


NA MAGENDELA HAMISI, MOROGORO

WAKALA wa Usajili wa Leseni za Biashara (BRELA), imewatahadharisha wafanyabiashara wa mtandaoni kusajili Alama za Biashara zao kwa lengo la kujipanga kuhimili ushindani wa soko huria Barani Afrika pindi litapofunguka.

Hayo amebainishwa leo, Juni 20, 2024 mkoani Morogoro na Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu kutoka BRELA, Loy Mhando wakati akiwasilisha mada inayohusu Miliki Ubunifu kwa baadhi ya waandishi wa Mkoa wa Dar es Salaam, wanaoandika habari za biashara wakati wa mafunzo ya kuwaongezea uwezo  ya namna ya kuripoti kwa usahihi taarifa kuhusu shughuli za taasisi hiyo.    

Amesema, changamoto kubwa ambayo inaweza kujitokeza pindi soko litakapofunguka, kama kuna 'mark' inatumika Tanzania, pia inatumika na mtu mwingine katika mataifa mengine bidhaa zao hazitaweza kuingia hapa nchini ikiwa tu kama alama itakuwa imelindwa na bidhaa hiyo haitaweza kwenda katika nchi hizo kama wao watakuwa wameilinda katika nchi zao.

“Kama kuna ‘mark’ iko Tanzania, pia kuna kama hiyo kwa bidhaa aina hiyo hiyo inamilikiwa na mtu mwingine Uganda ama Namibia soko linapofunguka maana bidhaa za Mtanzania hazitaweza kuingia kwenye mataifa hayo kwa  kuwa wao tayari wameilinda,

“Pia wao hawataweza kuleta bidhaa huku kwa kuwa huyu wa Tanzania kama atakuwa amelinda, kama hajalinda atashangaa kuona bidhaa za Namibia zenye 'mark' zinazofanana zinaingia hapa nchini na kuleta mkanganyiko, hivyo ni jambo la uelewa ili kuwaandaa wafanyabiashara waweze kuhakikisha wanaitumia IP ipasavyo ili kuepuka changamoto hiyo,” amesema.

Mhando ameongeza kuwa Alama za Biashara na Huduma ni nyenzo muhimu katika kuhimili ushindani kwenye soko na zina mipaka hivyo kama mfanyabiashara wa Tanzania, anataka alama yake itumike katika mataifa mengine ambayo atayaainisha atatakiwa kutukia mfumo kikanda utakaosaidia kudhibiti alama katika nchi hizo atakazopeleka bidhaa zake.


No comments:

Post a Comment