Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Christina Mwangosi na baadhi ya wasemaji wa Vyombo vya Usalama vya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Maafisa Habari wakiwa wameshika Kikombe na Cheti walichokabidhiwa leo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari baada ya Kuibuka mshindi wa pili katika utoaji wa taarifa kwa Umma katika kipindi cha mwaka 2023/2024.
NA MWANDISHI WETU
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo imekabidhiwa Kikombe na Cheti baada ya Kuibuka mshindi wa pili katika utoaji wa taarifa kwa Umma katika kipindi cha mwaka 2023/2024.
Wizara hiyo imeibuka na ushindi huo wa pili kati ya Wizara Kumi Bora na kati ya Wizara 26 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tuzo hizo zimekabidhiwa leo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati akifunga Kikao Kazi cha 19 cha Maafisa Habari wa Serikali, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment