Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Assembles Of God (TAG), Ilala Mission, Dkt Titus Mkama. (PICHA KWA HISANI YA MTANDAO MTEZA BLOG)
NA MWANDISHI WETU
IMEELEZWA
kuwa vijana ndio wanaovunja ndoa tofauti na wazee na hiyo inatokana na wengi
wao kuingia katika mahusiano hayo kwa tamaa za mafanikio bila kuchunguza kwa
kina tabia za mwenza wake.
Hayo
yamesemwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Assembles Of God (TAG), Ilala
Mission, Dkt Titus Mkama Mei 28 mwaka huu wakati akizungumza na Waandishi wa
Habari ofisini kwake Ilala jijini Dar er es Salaam.
“Shida kubwa
ambayo ipo ni vijana wengi kuingia katika ndoa bila kuwa na hofu ya Mungu na
kuvutwa na tamaa ya mafaniko ya uchumi ya mmojawapo na inapokuja kuwa tofauti
migogoro inapoanza.
“Tunapotaka
kuwafungisha ndoa tunawaambia kabisa ndoa huwa haivunjiki na biblia inakataa kuvunjika
kwa ndoa ila baada ya kufungishwa na kuona baadhi ya vitu haviendi sawa hawataki
kabisa kusikia kitabu cha dini kinasema nini wanasimamia msimamo wa kuvunja ndoa
tu.
“Na hapo
inakuwa ngumu kuwarejesha katika ndoa tofauti na wazee walio kwenye ndoa wengi
wao wakipata changamoto ukizungumza nao wanarejea katika mstari tofauti na
vijana wa dot com,” amesema.
Ameongeza
kuwa kinachotakiwa kwa vijana wanaotaka kuingia katika maisha ya ndoa kabla ya
kuchukua uamuzi huo wanatakiwa kumuomba Mungu ili awape mtu sahihi kwa ajili ya
ndoa .
Ameweka wazi
kuwa kanisa lake la Assembles of God Tanzania (TAG), Ilala Mission tangu
lianzishwe mwaka 1973 limefungusha ndoa zaidi ya 400 na anashukuru kuona ndoa nyingi za zamani
zikiendelea kudumu tofauti na za sasa.





No comments:
Post a Comment