UONGOZI CHUO CHA FURAHIKA WAONGEZA MUDA WA KUDAHILI WANAFUNZI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, June 28, 2024

UONGOZI CHUO CHA FURAHIKA WAONGEZA MUDA WA KUDAHILI WANAFUNZI


NA MWANDISHI WETU

UONGOZI wa Chuo Cha Ufundi Stadi cha Furahika chenye usajili namba VET/DSM/PR/2021/D169, kimeongeza muda wa dirisha la usajili wa wanafunzi wapya kwa muhula mpya wa masomo.

Kaimu Mkuu wa chuo hicho, kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam, Dkt David Msuya, amesema  usajili wa wanafunzi kwa muhula mpya unatarajiwa kufungwa Julai 5, mwaka huu na kutoa wito kwa wazazi ama walezi kuchangamkia muda huo ulioongezwa.

“Nawaomba wazazi au walezi  kuchangamkia nafasi hiyo adhimu kwa kuwaleta vijana wao wa kike na wa kiume kuja kuchukua fomu za kujiunga na masomo katika fani mbalimbali ikiwemo Umeme, Udereva, Hoteli, Bandari na nyinginezo”, amesema.

Aliongeza kuwa wanapokea wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali nchini ili kujiunga na kozi zinazofundishwa chuoni hapo hususan kwa vijana ambao walikosa nafasi ya kuendelea na masomo kutokana na changamoto za kimaisha ikiwemo kuwa na ufaulu hafifu kwa kidato cha nne au darasa la saba.

Alifafanua kuwa kwa wanafunzi ambao walipata alama hafifu katika mitihani ya kidato cha nne au walioshindwa kumaliza elimu hiyo au darasa la saba, wasione kuwa ndio mwisho wa kutimiza ndoto zao kielimu, Chuo Cha Furahiko kipo kwa ajili ya kutimiza ndoto zao kwa kupata elimu bure.

Amesema kuwa ili kutimiza ndoto za vijana katika nyanja ya elimu, Julai 25, 2024 watazindua maabara ya kisasa ya masomo ya sayansi hususan kwa wanaochukua fani ya umeme ambayo wataitumia kujifunzia na kupata uzoefu wa kutosha kabla ya kuhitimu kozi hizo.

“Wataitumia kwa ajili ya kufanya mazoezi ya vitendo zaidi ili kuwajenga utimamu wa kufanya kazi popote watakapokwenda baada ya kuhitimu na itakuwa maabara itakayotoa fursa kwa wanafunzi wa ndani na nje chuo kuitumia ili kuwaongezea maarifa na ujuzi.

Pia aliongeza kuwa kwa wanafunzi wa kozi hizo ikiwamo ya hoteli pindi wanapohitimu masomo na wanaofanya vema wanapata nafasi ya kutafutiwa ajira katika katika hoteli zilizoko jijini Dar es Salaam na mikoa mingine Tanzania Bara na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment