NA MAGENDELA HAMISI
WACHUMI nchini wameshauriwa
kufanya tafiti kwa ajili ya kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazoikabili
nchi kulingana na mazingira yaliyopo ili kuleta tija kwa Serikali kupiga hatua
stahiki hususan katika kuwasaidia vijana kuwa na uwezo wa kujiajiri au
kuajiariwa
Hayo yatatokana kuwa na uchumi imara
utakaosaidia vijana kuwa na uwezo wa kujiajiri ama kuajiriwa kutokana na kuzalishwa
ajira lukuki, hivyo wachumi wanapaswa kuisaidia Serikali kutatua changamoto
zinazoikabili katika sekta ya uchumi.
Hayo yamebainishwa leo, Julai 12,
2024 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa
Adolf Mkenda wakati akifungua Kongamano la Pili la mwaka 2024 la Uchumi (EST)
la Jumuia la Wachumi Tanzania.
Profesa Mkenda ambaye alimwakilisha
Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango ambapo alisistiza kuwa ikiwa wachumi hao
watafanya tafiti zao kulingana na mazingira ya nchi na kuishauri Serikali namna
ya kutatua changamoto za kiuchumi kwa maendeleo ya taifa.
“Nafasi ya wachumi ni kuhakikisha
wanachambua masula mbalimbali ya kiuchumi kitaalamu na kuibua changamoto
zilizopo na kuipa Serikali njia stahiki ya kufanya kwa lengo la kupata matokeo
mazuri,” amesema.
Amefafanua kuwa mageuzi ya uchumi
yatachochewa na tafiti nzuri zitakazofanywa na wachumi zitakazosaidia kuongeza ajira
kwa kundi la vijana ambalo linahitaji kusaidiwa ili kuwafikisha katika
matarajio yao kwa kushiriki katika uzalishaji mali jambo litakalofanikisha
ukuaji wa uchumi.
Amesema hadi sasa Serikali
imefanikisha kwa asilimia kutekeleza nyanja mbalimbali za kiuchumi na kuleta
mageuzi makubwa ya kwenye sekta ya elimu kwa kuboresha miundombinu inayosaidia
kupatikana kwa elimu bora kwa Watanzania na siku zijazo ni dhahiri itachagiza kuongezeka
kwa wataalamu wa uchumi nchini.
Naye, Kaimu Mwenyekiti wa
Baraza la Wachumi Tanzania, Dkt Tausi Kida, amesema kongamano hilo linaambatana
na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa jumuiya utakatoa fursa ya kuchaguliwa kwa safu mpya
ya uongozi.
"Kwa siku ya leo kutakuwa
na mada mbalimbali zitakazojadili kwa kina kuhusu mwenendo wa uchumi na baada
ya kuhitimisha mijadala mchakato unaofuata utakuwa ni wa kuchagua, Mwenyekiti
na Makamu wake na wajumbe,” amesema.
No comments:
Post a Comment