PURA, TPDC WAJIPANGA KUTANGAZA MAENEO YATAKAYOVUTIA WAWEKEZAJI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, July 12, 2024

PURA, TPDC WAJIPANGA KUTANGAZA MAENEO YATAKAYOVUTIA WAWEKEZAJI


 NA SALHA MOHAMED

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA), kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), wanatarajia kutangaza maeneo yatakayowavutia wawekezaji kwa ajili ya kuendeleza na kutafuta mafuta hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka 2025.


Utafiti unaonesha zaidi ya asilimia 50 ya ardhi ya Tanzania kuna miamba tabaka ya mafuta na gesi hasa katika ukanda wa Kaskazini Pwani kuanzia  Mkoa wa Tanga hadi Kusini na kuingia baharini zaidi ya km 400.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA), Charles Sangweni aliyasema hayo Julai 12, 2024 kwenye Maonesho ya 48 ya  Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


"Katika kuendeleza shughuli za utafiti, PURA tunategemea mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwaka ujao, tutatangaza maeneo mbalimbali ambayo tutavutia wawekezaji kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) kutafuta,kuendeleza na kutafuta mafuta,"amesema.


Amesema PURA imeshiriki maonesho ya Sabasaba mwaka huu kwa kuendeleza kauli mbiu ya maonesho hayo  inayosema 'Tanzania ni mahali sahihi pa uwekezaji.


Amefafanua kuwa PURA inatekeleza hilo kwa kujenga mazingira bora na yanayovutia wawekezaji ambao ni kampuni zinazofanya tafiti kwenye eneo la mkondo wa juu wa petroli.


"Katika mnyororo wa kuongeza thamani zao la petrol tuna mikondo mitatu, kuna mkondo wa juu unahusu kutafuta, kuendeleza na kuzalisha Petroli.


"Kuna mkondo wa kati petroli inapotoka inayokuwa kwenye mfumo wa tope huchakatwa na kutoa mazao yanayotoa petroli, dizeli na mafuta ya taa,"amesema.


Amesema kwa sasa dunia inabadilika, kwenye matumizi ya nishati, ambapo inazungumzia nishati safi inayozuia uchafuzi wa mazingira (Nishati jadidifu).


Mhandisi Sangweni ameongeza kuwa lengo ni kufikia mwaka 2060 dunia iwe imefikia matumizi ya nishati jadidifu kwa kiasi kikubwa.


Amesema Tanzania imeweka malengo ya kutumia nishati safi ya kupikia kwa kufikia hadi asilimia 80 ifikapo 2034.


Amesema PURA inatafuta gesi ambayo itasaidia kutumika katika maeneo mbalimbali yakiwemo nyumbani, kwenye gari, na kuendeshea mitambo.


"Gesi ya sasa iliyogundulika ya Songosongo na Mnazibay imepitishwa duniani kama chanzo cha nishati ambacho kitatumika kwa kipindi cha mpito kuelekea matumizi ya nishati jadidifu,"amesema. 

No comments:

Post a Comment