MKOA WA GEITA KUFUNGULIWA KWA BARABARA ZA LAMI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, August 13, 2024

MKOA WA GEITA KUFUNGULIWA KWA BARABARA ZA LAMI

Naibu Waziri wa Ujenzi,Injinia Godfrey Kasekenye akifafanua jambo kuhusu ujenzi wa barabara za lami mkoani Geita.

 MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Injinia Godfrey Kasekenya amhakikishia Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Serikali imepanga kufungua Mkoa wa Geita kwa barabara za lami ili kurahisisha huduma za usafiri na uchukuzi  hivyo kukuza uchumi wa mkoa huo.


Akizungumza na wananchi wa mji wa Katoro mkoani humo, Injinia Kasekenya amesema nia ya Serikali nikuhakikisha maeneo yote yenye uzalishaji na biashara kubwa yanafikika kirahisi kwa Barabara za lami ili kuleta tija na ufanisi kwa wananchi.


"Katibu Mkuu mwaka huu tumejipanga kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara za Nzera-Nkome Km 20, Mtakuja-Bukoli- Bulyanhulu-Busoka-Kahama KM 122.7 na Ushirombo-Katoro 58.3", amesema.


Pia amewataka wakazi wa Mkoa wa Geita kutumia  fursa ya ujenzi wa barabara hizo kupata  ajira na kukuza shughuli za biashara, uzalishaji na huduma ili kukuza uchumi binafsi na wa mkoa wa Geita kwa ujumla.



No comments:

Post a Comment