FURAHIKA NI CHUO KINACHOUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA – NAIBU WAZIRI ANNA PAUL - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, September 28, 2024

FURAHIKA NI CHUO KINACHOUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA – NAIBU WAZIRI ANNA PAUL


NA MWANDISHI WETU

IMEELEZWA kwamba Chuo cha ufundi Stadi cha Furahika ambacho kipo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam ni chuo kinachounga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan katika jitihada za kuwandeleza vijana kwa kuwapatia elimu bure.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar, Anna Athanas Paul, ameyasema hay oleo jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 16 ya chuo ambapo wanafunzi 220 wamehitimu masomo yao katika fani mbalimbali.

“Pongezi kwa Rais wetu, Dkt Samia kwa kutoa fursa hizi za elimu na pongezi pia kwa mkuu wa chuo hiki kwa kufanikisha vijana wetu ambao wamekosa fursa ya kuendelea na masomo kwa kukosa fedha ama sababu nyingine, kupatiwa elimu bure bila malipo yoyote.

 “Jitihada hizi zinazofanywa na uongozi wa chuo hiki wa kutoa elimu bure ni za kuigwa na watu wengine wanaopenda maendeleo ya nchi yetu na wanaowapenda kuona vijana wanafanikiwa kwa kuwaendeleza kielimu itakayowafanya waweze kujiajiri na kuachana kutegemea ajira za Serikali ambazo hazitoshi,” amesema.

Pia Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Elias Mpanda, amewaomba wazazi kuwapeleka vijana wao katika chuo hicho, kupata elimu bure ili kutumia vema, fursa ya Rais Samia ya kuendeleza kwa vijana wa kitanzania kielimu,  hususan waliokosa nafasi ya kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha.

“Ukiachana na hilo pia niwaombe wadau mbalimbali waiunge mkono Serikali kwa kuikisaidia chuo hiki kwa vifaa ambavyo vinavyohitajika ikiwemo cherehani, kompyuta na mengine jambo litakalosaidia vijana wengi kujiendeleza kielimu na kuwatoa katika makundi maovu,” amesema.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya, amesema kwamba katika mahafali hayo, wanafunzi 220 wamehitimu na sasa wanaenda katika soko la ajira na hana wasiwasi kwa maana wengi wao tayari wamefanikiwa kupata ajira baada ya kwenda ‘field’ na uwezo kuonekana na kupatiwa ajira.

“Sina shaka na hawa wahitimu kwani wengi wao tayari wameajiliwa Zanzibar, Arusha na hapa Dar es Salaam baada ya kwenda ‘field’ na wengine naamini wataajiliwa kwa maana wana uwezo mkubwa na watakaokosa watajiajiri,” amesema.

Ameongeza kuwa kwa kila mwaka malengo yao ni kupokea wanafunzi 400 hadi 500 ingawa idadi hiyo haifikiwi kutokana na wazazi wengi kushindwa kupeleka watoto wao katika chuo hivyo, anatoa wito kwa wazazi kupeleka vijana wao kwa ajili ya masomo katika muhula mpya na dirisha wa ajili ya udahiri liko wazi na watasoma bure na watakacholipia ni ada ya mtihani wa Serikali ambao ni shiringi 50,000 tu.













No comments:

Post a Comment