NA HAMISI MRISHO
MSIMU wa pili wa Guardians Of The Peak umefanikiwa kupata wanafanzi watano kati ya 42 kutoka Vyuo Vikuu hapa nchini ambao watakuwa mabalozi wa kuhamasisha Nishati Safi ya Kupikia katika maeneo yanayozunguka Mlima Kilimanjaro.
Wanafunzi hao wato ambao wamepatikana baada ya mchujo watajumuika na wadau wengine kupanda Mlima Kilimanjaro kuanzia Januari 20 hadi 31 mwaka huu lengo mahususi nai kuutangaza kimataifa na kuhamasisha uhifadhi wa mazingira kwa jamii zinazouzunguka mlima huo.
Akizungumza katika halfla
ya utangazaja wa jambo hilo, leo Januari 14, 2026 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Filamu, Emmanuel Ndumukwa, kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania (TFB) Dkt. Gervas Kasiga, amesema shughul hiyo itatilia mkazo umuhimu
wa nishati safi ya kupikia
Pia nashukuru kuona
wanafunzi wa vyuo nao kujumuishwa katika jambo hili muhimu kwa mustakabali ya
nchi yetu naamini watakuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha matumizi ya
nishati safi katika mlima Kilimanjaro ikizingatiwa kuwa kuna miti mingi ya
asili ambayo inazunguka mlima na inahitaji kulindwa.
Amesema kuwa katika msimu huu wa pili uzalishaji wa tamthilia ya (documentary series) Guardians of the Peak yamekamilika na jamii itajionea filamu itakayosimulia chagamoto kadhaa za uhifadhi wa mazingira katika mlima na namna ya kuzitatua ili kufikia malengo.
"Kupitia simulizi hiyo watajionea changamoto za kimazingira zinaukabili mlima huo na juhudi za Tanzania katika uhifadhi, pamoja na athari pana za mabadiliko ya tabianchi kwa vivutio vya asili duniani.”
Ameongeza kuwa msimu wa pili
unatarajiwa kuingia kwa undani zaidi katika uhalisia unaoukabili mlima mrefu
zaidi barani Afrika, kwa kuangazia juhudi za uhifadhi, ushiriki wa jamii
zinazouzunguka mlima huo, pamoja na mizani nyeti kati ya uhifadhi wa mazingira
na shughuli za utalii.
Amefafanua kuwa kupitia mchakato huo sauti ya Tanzania itapenya katika majukwaa ya kimataifa yanayohusu mazingira na filamu za maandishi, pamoja na kuimarisha taswira ya nchi kimataifa.
Pamoja na hilo amesisitiza kwamba Serikali itaendelea kuwezesha na kuunga mkono miradi inayotumia filamu kama chombo cha elimu, mabadiliko ya kijamii na kuitangaza Tanzania kimataifa.
Aidha, aliwahimiza
watayarishaji wa filamu, wasanii wa maonesho, taasisi za serikali, sekta
binafsi pamoja na vyombo vya habari kushirikiana na kuunga mkono Guardians of
the Peak na kazi nyingine zinazochanganya ubunifu wa kisanaa na maslahi ya
taifa na dunia kwa ujumla.





No comments:
Post a Comment