LWAKATARE AFICHUA SIRI YA KUTAKA KURITHI KITI CHA PROF. LIPUMBA CUF - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, September 3, 2024

LWAKATARE AFICHUA SIRI YA KUTAKA KURITHI KITI CHA PROF. LIPUMBA CUF


NA HAMISI MRISHO

ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF (Bara), Willfred Lwakatare (63), amesema kuwa kujitokeza kwake kuchukua fomu ya kugombea Uenyekiti imekuwa si kwa bahati mbaya bali ni kutokana na kuwa na nia thabiti na mikakati imara ya kukijenga chama hicho.

Hayo ameyabainisha jana wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake Kimara jijini Dar es Salaam na kufafanua kuwa harakati za kuwania nafasi hiyo alizianza tangu alipokuwa na umri wa miaka 35 katika uchaguzi ambao alishindwa kwa kura chache baada ya kushika nafasi ya pili kati ya wagombea saba.

“Niligombea uenyeketi Cuf kwa mara ya kwanza nikiwa na umri wa miaka 35 baada ya kushindwa nilimuuliza Maalim Seif ambaye kwa sasa ni marehemu sababu ya kupata matokeo hayo, aliniambia umri na uzoefu ingawa nilikuwa wa moto na kukubalika na wajumbe wengi na akashauri niendelee kujijenga nitafanikiwa siku za usoni nadhani ndio muda  umefika” amesema.



Lwakatare ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini kwa vipindi viwili kwa chama tofauti, amebainisha kuwa anauwezo mkubwa wa kupanga mikakati ya kukiweka chama katika nafasi nzuri ya kushinda chaguzi mbalimbali ambayo ndio malengo makubwa ya chama.

Mkongwe huyo ambaye ni miongoni mwa waasisi wa chama hicho amesema kama atafanikiwa kupata ridhaa ya wajumbe, kuongoza chama hicho atahakikisha kinakuwa cha kidigital kwa kuweka mfumo wa kusajili wanachama kupitia simu ya mkononi popote walipo na watalipa ada kwa njia hiyo hali itakayosaidia kukuza mapato.

Pia amekumbusha kwamba mikakati yake ya kukifanya chama kuwa imara zilianza tangu akiwa Naibu Katibu Mkuu, alipofanikisha kununuliwa jengo la chama hicho ambayo kwa sasa ndio Makao Makuu yalipo Buguruni jijini Dar es Salaam  na kutoka kupanga katika nyumba ya wageni ambayo ndio walikouwa wakiendesha shughuli zao chama hapo awali.

“Naijua Cuf vizuri tofauti na vyama vingine, hivyo naamini nikipata nafasi ya kuwa mwenyekiti nitafanya mengi ya kukiimarisha chama na nitatengeneza chama cha siasa ambacho hakijawahi kuwepo hapa nchini na uwezo huo ninao,” amesema.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Kitengo Cha Uchaguzi Wilaya ya Temeke chama hicho, Shilingi Hashim, Uchaguzi Mkuu wa utafanyika baada ya chaguzi za Serikali za Mitaa kutamatika.

"Sababu kubwa ya kufanyika baada ya chaguzi za Serikali za Mitaa kutamatika ni kutokana na chaguzi ndani ya chama kufanyika karibukaribu ukiwemo uchaguzi wa vijana, wa akina mama , wazee hivyo kuwakusanya pamoja inakuwa ni kazi kubwa ndio tukaona tuupeleke mbele kwa maslahi ya chama.

"Pia tumeupeleka mbele ili kutoa nafasi ya wagombea nafasi ya uenyekiti waliopembezoni mwa nchi nao wapate nafasi ya kuwania ili kuleta ushindani na kupata kiongozi sahihi,"amesema.



No comments:

Post a Comment