MCHENGERWA AWAPA MAAGIZO MAZITO DART, UDART - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, September 2, 2024

MCHENGERWA AWAPA MAAGIZO MAZITO DART, UDART

 


NA MAGENDELA HAMISI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, ameagiza Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) na Wakala wake (DART) hadi kufikia Desemba mwaka huu wawe wamenunua mabasi 670.

Ameongeza kuwa mchakato huo utasaidia kutosheleza utoaji wa huduma ya safari jijini Dar es Salaam kwa maana wananchi wamechoka kusubiri huduma hiyo kwani baadhi ya barabara za Mwendokasi tayari zimekamilika ikiwemo ya Mbagala ambayo inahitaji mabasi 500 na Morogoro ikihitaji 170.

Mchengerwa ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mageti Janja na Kadi Janja ambazo zitatumika kufanya malipo ya nauli katika usafiri wa mabasi yaendayo haraka hali itakayosaidia kujibu maswali ya watanzania kuhusu changamoto za usafiri wa mwendo kasi.

“Ongezeni ubunifu kwa katika jambo hili ikiwezekana wakaribisheni Watanzania kushiriki katika zabuni ya kuhudumia mabasi ya Mwendokasi, naamini watanzania wanaweza kwani zipo kampuni zina mabasi zaidi ya 300 na kama watashirikishwa tutafanikiwa, hakuna haja ya kusubiri wawekezaji wa nje.

“Pia kwa sasa kuna reli ya SGR kutoka Dar kwenda Dodoma ni imani yangu abiria katika mabasi watakuwa wamepungua kwa asilimia kubwa, hivyo mkizungumza na wamiliki wa mabasi wanaweza kufanya makubwa katika mwendokasi, kama wameweza kuhudumia watanzania kwa kupeleka mabasi mikoani hawawezi kushindwa kuhudumia Dar es Salaam,” amesema.

Awali akizungumzia uzinduzi wa Mageti janja na Kadi Janja, amesema pongezi ziende kwa Dart kutokana na kuja na mfumo huo ambao unakwenda kujibu maswali ya namna ya ukusaji nauli kwa kuachana na karatasi na kuanzia kesho kadi zitaanza kutumika ni mapinduzi makubwa katika huduma uya usafiri.

Ameongeza kuwamfumo huo wa kutumia kadi unafanya usafiri wa mwendokasi kuwa katika kiwango cha juu, “ hivyo niwapongeze Dart kwa kutekeleza agizo la Kamati ya Bunge na dhamira ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kujibu hoja kwa wananchi katika changamoto zilizokuwa zikiwabili katika ulipaji wa nauli.

Pia amesisitiza kwa Dart kuhakikisha wanawachukulia hatua kali madereva wanaokwenda kinyume na sheria na taratibu ikiwemo kuacha abiria katika vituo, ilihali mabasi yao yakiwatupu na wale wenye lugha chafu kwa abiria.

Amesisitiza kuwa kwa watendaji wa Dart, wanatakiwa kuhakikisha wanaondoa changamoto ya abiria kukaa vituoni kwa muda mrefu kwa maana imekuwa ni kero ya muda mrefu licha ya kuwekwa utaratibu mzuri muda wa kufika na kuondoka kwa mabasi vituoni ingawa imekuwa ni tofauti na kuzusha malalamiko kwa abiria.

Mchengerwa , pia alitoa wito kwa Dart kuhakikisha kadi hizo zinapatikana kwa urahisi na isiwe kuna changamoto katika upatikanaji wake ili kuondoa malalamiko yasiyo ya msingi kwa wasafiri.

Tofauti na hilo Mchengerwa aliwataka Dart kuunganisha mfumo wa kadi hizo na mifumo mingine ili kufanya kila mtumiaji awe na kadi moja tu.

Naye Mtendaji Mkuu wa Dart, Dk Athumani Kihamia, mfumo huo unakwenda kuwa na faida kubwa pindi utakapoanza kutumika baada ya kuzinduliwa na mojawapo ni utaondoa kero wa urudishaji chenji kwa abiria.



Pia ameongeza kuwa mfumo huo unakwenda kuondoa foleni iliyokuwepo kwa abiria wakati wa kukata tiketi  na itafanikisha abiria kuingia kwa haraka kwenye mabasi hayo na kuanza safari.

“Tofauti na hayo mfumo huu unakwenda sambasamba na mfumo wa uongozaji mabasi na nidhahiri tunakwenda katika mamafaniukio makubwa, amesema.



No comments:

Post a Comment