NA HALIMA MWAMBA
MAMA Mzazi, wa aliyekuwa msanii wa uigizaji nchini, Steven Kanumba, Flora Mutegoa, amewapongeza waandaaji wa Tamasha la kuwambuka na kuwaombea dua wasanii ambao wametangulia mbele ya haki.
"Tamasha hili linafanyika kwa mara ya kwanza tangu, mwanangu afariki, hivyo niwapongeze sana waandaaji kwani tunaowakumbuka leo hatupo nao kimwili lakini kiroho tuko nao, hivyo ni jambo la faraja kuwakumbuka," amesema.
Pia niamshukuru Mungu kwa Kuwapa Maono ya kuandaa tamasha hili kwani ni miaka 12 Sasa tangu mwanangu Kanumba afariki dunia na Leo ndio nashuhudia tamasha la namna hii, amesema.
No comments:
Post a Comment