SERIKALI YATENGA BIL. 3 KWA WASANII - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, September 7, 2024

SERIKALI YATENGA BIL. 3 KWA WASANII


NA HAMISI MRISHO

SERIKALI Kwa mwaka huu wa fedha imetenga Shlingi bil 3, kwa ajiri ya kutoa mikopo kwa wasanii wa kazi za uigizaji nchini kwa lengo kujiendeleza kwenye shughuli zao.


Hayo yamebainishwa leo Septemba 7, 2024 na Mshauri wa Rais, Angela Kahiruki katika shughuli ya dua ya kuwakumbuka wasanii ambao wametangulia mbele ya haki, ambayo imepewa kaulimbiu inayosema 'Faraja ya Tasnia Tutawakumbuka Daima'.

"Kikubwa ambacho naweza kusema kwa wasanii kutumia vizuri mikopo inayotolewa na Serikali kwaajili ya kuendeleza vipaji vyenu na kuinua tasnia filamu nchini ili kuleta tija stahiki.

 

Pia amesema amewataka wasanii kuhakikisha wanarejesha mikopo kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine mikopo kama ambavyo imekuwa katika msimu uliopita.


No comments:

Post a Comment