BENKI ya TCB imekabidhi mabati 250 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kusaidia maendeleo na kurudisha shukrani kwa jamii.
Hafla ya kukabidhi mabati hayo imefanyika leo
wilayani humo na imeongozwa na Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano ya Umma, Chichi Banda, na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa Serikali, wananchi na wawakilishi wa benki hiyo mkoani Tabora.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Banda, amesema wanayofuraha kutoa msaada huo ikiwa ni sehemu
ya kurudisha shukrani kwa jamii na wanaamini kwamba ni kichocheo cha kuboresha maendeleo
wilayani humo.
“Tunafurahia kutoa mabati haya kwa Halmashauri
ya Wilaya ya Uyui, lengo letu ni kusaidia katika miradi ya maendeleo ambayo
itaboresha maisha ya wananchi.
“Tunaamini
kuwa rasilimali hizi zitakuwa na manufaa makubwa katika ujenzi wa miundombinu
na huduma za jamii, amesema.
Mabati
hayo yamepangwa kutumika katika ujenzi wa shule, vituo vya afya, na nyumba za
makazi na kusaidia kuboresha mazingira ya maisha na elimu kwa jamii.
Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, inasisitiza
umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ili kufanikisha
maendeleo endelevu.
“Tunawakaribisha
wananchi kushiriki katika miradi hii, na tunatoa shukrani zetu za dhati kwa
Benki ya TCB kwa mchango wao mkubwa. Huu ni mfano mzuri wa namna sekta za Serikali
zinavyoweza kusaidia katika maendeleo ya jamii,” amesema Venance Protas (MB).
Hafla
hiyo ilikamilika kwa burudani mbalimbali na wananchi wakitoa shukrani zao kwa benki
ya TCB kwa kutoa msaada huo ambao wanaamini utaleta tija katika kuleta
maendeleo ya Halmashauri ya wilaya hiyo kwa kusaidia kuboresha huduma na maisha
ya wananchi wa Uyui kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment