WAANDISHI WATAKIWA KUANDIKA HABARI ZA LISHE KWA KUFUATA VYANZO SAHIHI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, September 27, 2024

WAANDISHI WATAKIWA KUANDIKA HABARI ZA LISHE KWA KUFUATA VYANZO SAHIHI


NA MWANDISHI WETU


WAANDISHI wa Habari nchini wametakiwa kutafuta taarifa sahihi kutoka kwenye vyanzo,chombo ama taasisi 



husika ili kufanikisha kuandika kwa usahihi masuala yanayohusu lishe ili kufikisha ujumbe stahiki kwa wananchi pasipo kupotosha.



Ofisa Uhusiano na Mtafiti wa Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Hamza Mwangomela,a mebainisha hayo Septemba 26, 2024 jijini Dar es Salaam wakati semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari namna ya kuandika habari kwa usahihi kuhusu masuala ya lishe.


   




"Kuna mambo yanajitokeza hususan katika mahojiano utakuta anahojiwa mtu ambaye si sahihi na kusababisha kupotosha usahihi wa jambo husika na inapotokea hivyo tunachukua hatua za kuwaita 


walihojiwa ili kufahamu wanachokijua kuhusu lishe na wengi wao tunabaini hawana elimu ya kutosha"




"Pia hatuishii hapo huwa tunawaandikia barua vyombo husika kwa hatua zaidi ili kupata maelezo ya kutosha na wale wakaidi, tunapeleka taarifa zao katika mamlaka zinazowadhibiti ikwemo, Mamlaka za Mawasiliano Tanzania (TCRA)na tunashukuru mambo yanakwenda vema," amesema.




Mwangomela amesema jambo lingine ambalo baadhi ya waandishi na watangazaji wakosea wakati kutumia neno kirutubisho na kirutubishi litumika kwa binadamu.




Akifafanua hilo, Mwengomela amesema " Neno kirutubisho usahihi wake ni kwamba linatumika kwenye mimea na neno Kirutubishi linatumika kwa binadamu.



No comments:

Post a Comment