NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha ACT Wazalendo kimetoka wito kwa Ofisiya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kurekebisha kasoro tatu ambazo zimejitokeza katika Maandalizi ya mchakato WA uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Chama hicho leo, jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema kwamba wakati mchakato wa, uchaguzi huo ukiendelea wamebaaini kasoro tatu ambazo ametaka zifanyiwe kazi mapema kabla hazijaleta madhara
Moja ni kwamba tumebaini upande wa mawakala kuna udhaifu mkubwa ambapo baadhi ya halmashauri zinataka waapishwe katika makao makuu na nyingine zinataka waapishwe kwenye Ofisi za Kata.
Pia zitaka kuwaapisha siku moja kabla ya mchakato wa mchakato wa uchaguzi kuanza jambo ambalo linawanyima muda wa kutosha kwa vyama kuandaa mawakala.
Amedai hiyo inaonekana kama vile vyama vinaviziwa ili vishindwe kuaandaa mawakala kwa wakati.
Ado amesema kasoro ya pili ni katika Kamuni inayosimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa kurujusu TAMISEMI, kuwaapisha mawakala WA ngazi ya Msimamizi wa Kituo au ya juu yake ilhali uchaguzi huo ni wa ngazi Mitaa, vitongoji na vijiji.
Ameongeza kuwa hali hiyo inafanya kuwepo mkanganyiko kama vile mchakato huo wa uchaguzi hauna uongozi.
Amedai kasoro nyingine ambayo wamebaini ni kutokuwepo kwa muunganiko wa kitaifa, ingawa awali walitoa maoni yao kwa TAMISEMI kwamba katika ngazi ya kitaifa kuna Msimamizi ambaye ni Waziri husika ambaye ana viongozi wake wa kitaifa.
Amesema waliamini kwamba kila hatua wangekuwa wanashirikishwa kama vyama na wao kama makatibu wangekuwa wanashusha taarifa ngazi za chini.
"Kutokana na kasoro hizo tunatoa wito kwa TAMISEMI kufanya mambo matatu, moja .... Waziri wa TAMISEMI, hasikae mbali na Vyama vya Siasa, na tamisemi isifanye uchaguzi Kwa kuviziana na tunataka kila hatua iliyo kwenye kalenda ya uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi ashirikishe vyama.
"Pili, tunaipa wito tamisemi katika kipindi kisichopungua siku saba kabla ya mchakato wa uapishaji wa mawakala iwe imeshusha taarifa kwa viongozi wa ngazi husika ili ifahamike mawakala wanaapishwa wapi na kwa utaratibu gani.
"Tatu, Tamisemi ihakikishe uchaguzi wa Serikali za Mitaa,mambo yake yanafanyike katika ngazi ya msingi ambayo ni katika kitongoji,kijiji na mtaa.
Pia , Ado akatoa wito kwa watanzania wote kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la Mkazi ili kupata fursa ya kupiga kura .





No comments:
Post a Comment