BRELA YAWAITA WENYE VIWANDA, KAMPUNI KWENDA KUSAJILI BIDHAA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, October 1, 2024

BRELA YAWAITA WENYE VIWANDA, KAMPUNI KWENDA KUSAJILI BIDHAA


NA SOPHIA KINGIMALI

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka  wenye viwanda na makampuni kusajili bidhaa zao ili waweze kutangaza bidhaa zao kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.


Akizungumza Octoba 1,2024 katikà Maonesho ya pili ya Kimataifa ya Viwanda Nchini yaliyofanyika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es Salaam, Ofisa Leseni BRELA, Ndeyanka Mbowe, amesema wapo hapo kwa ajili ya kusajili viwanda na biashara na kutoa elimu kwa jamii ijue umuhimu wa kusajili bidhaa zao ambapo huduma hiyo pia inapatikana kwenye maonesho hayo.


Mbowe amesema toka mwaka 2018 walianza shughuli za  usajili kwenye viwanda huku wakiwa wanaendesha  shughuli hizo kisasa.


"Tulianza mageuzi kwenda kidigitali na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa wenye viwanda na kampuni hivi sasa wanasajili  bidhaa zao mtandaoni,”amesema.


Hata hivyo amesema BRELA imejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa jamii ili kujua umuhimu wa kusajili viwanda  kampuni.


“Ukisajili kampuni au kiwanda unakuwa na nafasi kubwa ya kushiriki maonesho ya ndani na nje ambayo yanatoa fursa ya kutangaza bidhaa yako,”amesema .


Aidha  Mbowe ametoa wito kwa wenye viwanda kusajili viwanda vyao ili kujiwekea mazingira mazuri kibiashara


Sambamba na hayo amesema bado kuna mwitikio hafifu katika maonesho hayo hivyo wamewataka wenye viwanda na kampuni kuendelea kusajili bidhaa zao na kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye maonesho kwani yanatoa fursa ya kupata elimu na kubadilishana uzoefu.


Aidha Mtandao huu wa habari wa Fullshangwe  lilishuhudia baadhi ya wananchi wakifika katika banda hilo kupata elimu ya kusajili viwanda vidogo,kati na vikubwa huku wakionesha kuridhishwa na huduma waliopata.


“Leo nimeelewa kazi za BRELA kutokana na elimu niliyoipata kutoka katika maonesho haya ambayo yamenivutia na mimi kuanzisha kiwanda changu kidogo.


"Kwa sababu si ghali kusajili kiwanda na nikisajili nauhakika nitapata  fursa mbalimbali za kutangaza bidhaa yangu ninayouza,”amesema Godwin Claudi .


Naye Plakseda Luis amesema yeye amefanikiwa kuwa na kiwanda kidogo lakini biashara yake ilikuwa haiendi vizuri kwa sababu alikuwa hajaisajili.


“Nilivyopata elimu kutoka BRELA niliweza kusajili biashara yangu na sasa hivi ninashiriki maonesho mbalimbali kwa lengo la kutangaza bidhaa ninazouza,”.amesema.




No comments:

Post a Comment