NA MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewataka Watendaji na Watumishi katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati kuwa na umoja, ushirikiano na ubunifu ili kusogeza huduma bora kwa wananchi ikiwemo za umeme, mafuta na Nishati Safi ya Kupikia.
Amesema hayo, Oktoba 28, 2024 jijini Dodoma wakati wa kikao chake na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake ambacho ni cha pili kutoka uanzishwe mfumo mpya ndani ya Wizara na Taasisi zake wa kujifanyia tathmini ili kuona namna inavyofanya kazi ya kuhudumia wananchi.
No comments:
Post a Comment